Friday, August 5, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 9 & 10

MTUNZI:EDDAZARIA G.MSULWA

Tukavaa nguo zetu haraka haraka baada ya kuona tupo sawa nikachungulia dirishani na kumuona John akiwa amejishika kiuno huku hajui wapi tulipo
“Oya John sisi tupo huku”
“Ahhh mwanagu hukuwa unanisikia kipindi ninakuita au?”
“Sijasikia bwana tatizo lako wewe unawenge sana”

Nilizungumza huku nikitoka katika chumba tulichokuwa huku nikiwa na trey nne sisizo na mayai.Nikaingia katika banda la kuku na kuchukua kindoo kidogo kilicho na mayai kisha nikatoka nacho na kuanza kupanga yai moja baada ya jengine huku Madam Rukia akitoka akiwa ameshika trey mbili zisizo na mayai

‘”Wewe mbona umesimama humsaidii mwenzako katika kupanga mayai”
“Madam hapa nilipo nimechoka kama nini ninaogopa ninaweza nikayavunja hayo mayai ikawa ni kesi juu ya kesi”
John alizungumza huku akiwa anatafuta sehemu ya kukaa kabla hata hajakaa akasikia redio ya madam ikitoa sauti ya mziki.

“Umeme huo umerudi ngoja nikamalizie mechi yangu”
John akatoka mbio na kutuacha mimi na madam tukicheka kwani kwa vitendo anavyovifanya John ni sawa na mtoto mdogo wa kidato cha kwanza
“Hivi huyu mwenzako anaakili nzima”
“Ndio tena ndio anayetushikia darasani”
“Ehhee makubwa basi mshauri akue aache utoto”
“Sawa”

Tukaendelea na kazi ya kuyapanga mayai kwenye tery huku mara kwa mara tukiwa tunatazamana kwa macho ya wizi wizi.Tukamaliza tukasaidiana kuzibeba trey hizo hadi kwenye meza ya sebleni kwake

“Alafu Eddy kama utahitaji kuoga bafu hilo hapo kwani ninakuona unatokwa na jasho”
“Sawa madam….Vipi chai tunakunywa au ndio siku inapita kavu?”
“Ngoja niwachemshie mayai mangapi mangapi yatawatosha?”
“Kumi kumi”
“Eddy mwenzako anakazi ya kuakia wakati hata kuokota yai hata moja kwenye banda hajaokota”
“Mwaya madam usimsikilize huyu mayai mawili mawili yanatutosha”

Madam akaondoka akaingia kwenye chumba nikagundua kitakuwa ni jiko kwani nilisikia akigonganisha visufuria vinavyoonekana vimewekwa kwenye mpangilio usio mzuri.Nikaingia katika bafu aliloninyesha Madam Rukia nikavua nguo zangu na kufungua maji ya bomba la mvua nikabaki nimesimama huku mawazo juu ya ndoto niliyo iota yakanijia upya.

“Hivi si nilienda kuoga baada ya kupanda kitandani?”
Sikuwa na kumbukumbu za kutosha kama wakati nilipo panda kitandani kuupumzisha mwili wangu nilikwenda kuoga au usingizi ulinipitia na kuanza kuota vitu vya ajabu.Nikasimama kwenye mchuruziko wa maji kisha nikaanza kujisugua kila kona ya mwili wangu.Nikamaliza kuoga na nikamuomba Madam anipe msaada wa wa taulo la kujifutia maji.Akampa John na akaniletea bafuni,Nikajifuta maji kisha na kuvaa nguo zangu za shule,sikuwa na jinsi zaidi ya kuzivaa hivyo hivyo japo zina nuka jasho kwa mbali

Nikarudi sebleni na kumkuta John akiwa anaendelea kunywa chai,nikajumuika naye.Tukamaliza kunywa chai.Nikamuomba Madam Rukia anipatie japo pafyumu ili mwili uishiwe na kajiarufu ka jasho ambacho kalianza kunikera
“Ingia ndani kwangu utakuta dressing table utachagua ni pafyumu gani unayohitaji”

Nikaingia chumbani kwa Madam Rukia na nikaanza kutafuta ni pafyumu gani nitaweza kupulizia kwa bahati nzuri nikakuta body spry kama yangu.Nikaanza kujipulizia taratibu huku nikiwa nimefungua vifungo vya shati ili niweze kujipulizia katika makwapa vizuri huku nikiwa ninacheza.Mlango ukafungulia na Madam Rukia akaingia na akaanza kunishangaa kwa jinsi ninavyo cheza cheza.

“Kumbe wewe na rafiki yako akili yenu ni moja?”
“Kwanini Madam?”
“Kinacho kuchezesha chezesha hapo wewe ni kipi wakati wezako tunakusubiri?”
Nikanyamaza kimya,Madam Rukia akapiga hatua na kunifuata na kuanza kunifunga vifungo huku akinitazama usoni
“Mery anaonekana ana faidi”
“Ana faidi nini?”
“Ahaaa hakuna kitu”

==> Endela nayo <<kwa kubofya hapa>>
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )