Tuesday, August 9, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya13 & 14

MTUNZI:EDDAZARIA G.MSULWA

 .....Machozi yakaanza kunitiririka kwa wingi huku moyo wangu ukijawa na maumivu ni kwanini nilizungumza kitu kama kile,nikautoa mkono wangu koo ni mwa mama na kumkumbatia na kukiweka kachwa chake begabi mwangu na kuanza kumbembeleza taratibu.

“Eddy mwangu kwa nini unataka kuwa kama huyu baba yako?”
“Mama ninakuomba unisamehe sio kusudio langu kuzungumza hivyo”
 
Nikaendelea kumbembeleza mama taratibu hadi akanyamaza na taratibu usingizi ukaanza kumpitia baada ya muda kidogo akalala,Nikachukua shuka lake na kumfunika vizuri kisha nikatoka ndani ya chumba chake huku nikizima taa ya chumbani kwake na kushuka gorofani na kukaa kwenye sofa huku maneno ya mama akiwa anazungumza na dokta yakaaza kunirudia taratibu katika akili yangu huku yakiwa yanapita kama kanda wa video aina ya VHS.Kitu kinacho niumiza kichwa sana ni nani baba yangu na kitu kingine watu wengi wanasema ninafanana sana na baba yangu.

“Au mama atakuwa amechoka ndio maana akazungumza hivi?.........ila hata kama ni kuchoka itakuwaje akamwambia daktari mtu asiye husika katika familia yetu?”

Nikaendelea kujiuliza maswali yasiyo na majibu kiasi ya kujikuta taratibu nikiaanza kupitiwa na usingizi na kujikuta nikilala kwenye kochi.Nikaanza kuisikia sauti ya mama kwa mbali ikiniita taratibu huku akionekana akiomba msaada,Nikayafumbua macho yangu na kuuta mlango wa kuingilia hapa sebleni nikatazama nje na kukuta bado kuna giza jingi.

Nikanyanyuka kwa haraka na kwenda chumbani kwa mama nikakuta mlango wake ukiwa wazi nikaingia na kukuta kuna mwanaume yupo juu yake akimkaba huku kichwani kwake akiwa amevaa maski(Kinyago).Nikachukua chombo cha udongo kilichowekewa uwa la pambo na kwenda kumpiga nalo la kichwani na akaangukia kwa pembeni baada ya kuniona mimi akachomoka na kukimbia sikumjali zaidi ya kumuangalia mama kama yupo sawa au laa.Mama akanyanyuka huku akiwa anakooa huku akiwa amejishika koo.

“Mama unajisikiaje?”
“Vizuri mwangu fungua hiyo droo yangu ya kabati na unitolee bastola yangu”

  Nikafanya hivyo na kuitoa bastola yake kisha mama akanyanyuka kitandani na kuvaa raba zake za kufanyia mazoezi na taratibu tukaanza kutoka ndani kwa umakini wa hali ya juu huku na mimi nikifuata kwa nyuma.Tukashuka chini na kutoka nje kabisa ambapo kwa safari hii mlango ulikuwa umefungwa.Tukazunguka nyumba nzima kutazama kama kuna usalama kwa bahati nzuri kuna usalama.Tukaelekea getini ambapo hukaa askari ila hatukumkuta na wala hapakuwa na kitu chochote kinacho ashiria kuna tatizo lililo tokea katika eneo hilo.“Eddy kimbia kaniletee simu yangu ndani.”

  Nikaanza kujikongoja kongoja huku nikipiga hatua za haraka nikaamini kuwa mama amesahau kuwa mimi ni mgonjwa.Nikapanda ngazi kwa mwendo wa haraka kidogo kitendo cha kushika kitasa cha mlango wa kuingilia chumbani kwa mama nikasikia milio mitatu ya risasi ikitokea nje.Nikabaki nikiwa nimesimama huku miguu yote ikiwa inaanza kuishiwa na nguvu.Nikaaona hakuna haja ya kuingia ndani kuchukua simu moja kwa moja nikakimbilia jikoni na kuanza kukitafuta kisu ila sikukiona zaidi ya kuona Umma wa kulia chipsi,nikiona unanitosha kwenda kupambana na kitu chochote bitakacho kutana nacho nje.

 Nikafungua mlango na kujikuta mapigo ya moyo yakianza kuenda mbio huku wasiwasi ukiinza kunikamata mwili wangu kwani katika sehemu nilipomuacha mama sikumuona,Nikajikuta ninaaza kupata kiwewe cha miguu kila nikijaribu kusogea mbele ninajikuta ninashindwa sasa sikujua ni woga ndio unachangia kwani sikujua ni wapi mama yupo.Nikiwa bado nimesimama nikasikia mlio mwengine wa risasi ukitokea nje ya geti kwa mshtuko nusu nijikojolee kwani sikujua huo mlio ni nani aliyepigwa nao kwani kipindi nipo mdogo mara kwa mara baba alikuwa akinifundisha jinsi ya kutambua milio ya risasi pale inapokuwa imempiga mtu au kumkosa na moja kwa moja mlio niliousikia nikajua moja kwa moja risasi iliyolia imetua kwenye mwili wa mwanadamu.
   
 Nikajikaza kiume na kuanza kupiga hatua za kwenda nje ila kwa umakini huku uma wangu nikiwa nimeushika kwa umakini wa hali ya juu huku nikiwa makini kwa chochote kitakachojitokeza huku mwili mzima jasho lilinimwagika.Nikafungua geti dogo taratibu huku nikiwa nimetanguliza kichwa,Nikamkuta mama akiwa amesimama na askari kama watano wakiwa na bunduki zao mikonini huku kukiwa na mtu mmoja akiwa amelala chini huku mwili wake ukiwa unavuja damu nyingi.Nilicho kikumbuka kwa haraka haraka ni nguo alizo zivaa mtuu huyo na kukumbuka ni yule mtu niliyempiga na bakuli la dongo lililo kuwa na uwa la pambo.

“Alafu bado kijana mdogo sana”
“Ndio huyu nahisi ametuwa na mtu wa humo ndani kwako kwa maana haiwezekani ajiamini kiasi kwamba ya kujua moja kwa moja chumani kwako”
“Hilo usemalo litakuwa na ukweli ndani yake”.

 Mama akaendelea kujadiliana na askari wanaolinda eneo tunaloishi akiwemmo na askari wetu huku mama akimshushia lawama askari wetu ni kwa namna gani mtu anaingia ndani pasipo yeye kufahamu,askari wengine wakaja na gari lazo na kuchukua maiti huku wakimchukua askari wa getini kwetu kwenda kumuhoji maswali.


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )