Friday, August 5, 2016

Tundu Lissu afikishwa tena Mahakamani


HATIMAYE Jeshi la  Polisi Jijini Dar es salaam limemfikisha rasmi kizimbani Mwanasheria Mkuu wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo Singida Mashariki wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Tundu Lissu ambaye alikamatwa Juzi mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara Ikungi, Singida na kusafirishwa usiku, kulazwa Chamwino Dodoma na kufikishwa Dar jana saa saba mchana alilazwa rumande kabla ya kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mchana wa leo.

Akionekana mwenye kujiamini, Lissu amewasili Mahakamani Kisutu akitokea mahabusu ya Kituo kikuu cha Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam saa nane na dakika arobaini na nane (14:48) akiwa kwenye gari yenye namba za usajili  T 517 BET Corolla na akisindikizwa na ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Muda wowote kuanzia sasa, atapandishwa kizimbani ili kusomewa mashitaka ambayo yanatajwa kuwa huenda yakawa ni ya uchochezi kufuatia kauli aliyoitoa mahakamani hapo 02 Agosti Mwaka huu wakati akitoka katika kesi nyingine ya uchochezi inayomkabili.


Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )