Monday, August 22, 2016

VIDEO: Mbatia Amshangaa Magufuli ‘Kuwaziba Midomo ’ Wapinzani

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema kitendo cha Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli  kuendelea na mikutano ya kisiasa mikoani na kuwazuia viongozi wa vyama vingine vya siasa ni kutaka kukwamisha demokrasia nchini.

Akizungumza jana katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na Televisheni ya Azam, Mbatia alisema Rais Magufuli akiwa Singida, aliviponda vyama vya upinzani kuwa vimekufa.

“Akiwa Singida Magufuli alisema vyama vya siasa vya upinzani vimekufa na kuvilinganisha na nyoka aliyekanyagwa kichwa na kubakiwa na mkia tu unaocheza cheza,” alisema.

Alisema Agosti 12, mwaka huu Magufuli alikuwa mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam  akizungumza na wanachama wake  na kuonyeshwa na televisheni mbalimbali akikijenga chama chake.

“Nani anakwenda kuweka rekodi vizuri huko mikoani  kwa anayoyasema Magufuli kama anazuia wapinzani wasifanye siasa? Kwa hiyo yeye anajenga chama chake lakini anazuia wapinzani wasifanye hivyo,” alisema.

Alisema ikumbukwe kuwa Tanzania ni ya watu wote na wanatakiwa kufuata sheria na utaratibu uliowekwa na si vinginevyo.

Msikilize hapo chini akiongea

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )