Thursday, September 22, 2016

ACT- Wazalendo Wafuta Kongamano la Kidemokrasia Walilokuwa Wamepanga Kulifanya Kesho Kutwa........Sasa Kufanyika Oktoba 8


1. Katika kikao chake cha tarehe 05 Septemba 2016, pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo iliazimia kuwa Chama kifanye Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia (National Democratic Congress) tarehe 24 Septemba 2016 jijini Dar es Salaam.

2. Tangu kutangazwa kwa umma kuhusu mipango ya kufanyika kwa mkutano huu, wanachama wetu wengi na wananchi kwa ujumla, wakiwemo baadhi kutoka mikoani wameonesha nia ya kushiriki. Ili kuwapa fursa viongozi, wanachama na wananchi kushiriki kwenye mkutano huu, Chama kimesogeza mbele tarehe ya kufanyika kwake hadi tarehe 08 Octoba 2016.

3. Wanachama na wananchi ambao wangependa kushiriki kwenye mkutano huu watume majina yao na majimbo wanayotoka kwa namba 0653619906/0717047574. Ili kutoa muda wa kutengeneza vitambulisho vya washiriki, siku ya mwisho ya kupokea majina ya washiriki ni tarehe 01 Oktoba 2016.

4. Ikumbukwe kuwa mbali na kujadili masuala mbalimbali ya nchi na bara la Afrika, Mkutano wa Kidemokrasia ndiyo fursa pekee ya kikatiba ambapo mwanachama/mwananchi wa kawaida anayeshiriki anapata fursa ya kuwahoji ana kwa ana viongozi wa kitaifa wa ACT Wazalendo juu ya masuala mbalimbali ya Chama.

Ado Shaibu
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma
Imetolewa leo tarehe 22 Septemba 2016.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )