Friday, September 16, 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 5 & 6


Mwandishi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia....
.....Rahabu akapunguza mwendo wa pikipiki na agnes akaruka na kukimbilia njia aliyo kwenda kibopa,rahab akapita njia aliyo kwenda muntar.Muntar akajibanza kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla rahab akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa gongo la kifua na muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo mkononi....

Edndelea....
.....Rahab akanyanyuka haraka,akamtazama muntar ambaye alianza kucheka kwa dharau akimtazama rahab kuanzia juu hadi chini.Muntar akarusha gongo kwa kutumia nguvu nyingi,rahab akalikwepa na kurusha teke lililotua shingoni mwa muntar na akaayumba,kabla hajajiweka sawa rahab akampiga muntar ngumi kadhaa za kifua na kuzidi kumfanya muntar kuyumba mithili ya mtu aliyelewa kwa pombe za kienyeji.(mataputapu).

Muntar akajaribu kurusha ngumi ila rahab akafanya maamuzi ya haraka katika kuudaka mkono wake wa kulia,akajigeuza na kwakutumia bega lake akauvunja mkono wa muntar.Kilio cha maumivu makali kikamkumba muntar.Pasipo kuwa na huruma rahab akampiga mtama muntar na kumfanya aliachie gongo alilolishika.Rahab akaliokota gongo na kuanza kumpiga muntar gongo la kichwa hadi damu nyingi zikaanza kutoka nje kwa kasi kama bomba la maji lililo pasuka sehemu ndogo.

 Kibopa akafunga breki za miguu yake baada ya kukutana uso kwa uso na agnes.Kibopa akameza funda kubwa la mate huku mwili wake ukimtetemeka kiasi kwamba akabaki akiwa hajajua nini la kufanya.Agnes akaachia tabasamu pana baada ya kuiona surulia ya kibopa ikianza kuchora ramani ya kutota kwa mikojo aliyo shindwa kuizuia.
“ni....Iisssa...Mehe”

Kibopa alizungumza kwa kigugumizi kikali,agnes akapiga hatua hadi alipo simama kibopa na akamtisha kama anampiga ngumi ya uso,kwa woga uliokithiri ukammdondosha kibopa chini kama mzigo na akaanza kulia kama mtoto mdogo
“khaa wewe si jambazi,mbona unalia sasa?”

“mimi ni nilikuwa kibaraka waoo tuu,sioooo jambaazzziiii” kibopa alizungumza kwa kuyavuta vuta maneno kama amemeza fumba la uji wa moto na anashindwa kuumeza.Agnes akamtazama kwa huruma kipopa ambaye taratibu alianza kupiga magoti akimuomba msamaha.Agnes akampiga kofi la shavu kipopa na kumuamuru kusimama
“wenzenu wapo wapi?”
“wameshakufaa”
“changanya mbaliga zako,kabla sijabadilika”
“eheee....!!”

Agnes akampiga kibopa teke la makalio huku akimsindikiza na kofi la mgongoni na kumfanya kibopa aanze kukimbia kwa kasi kubwa.Agnes akabaki kucheka kwani hakutarajia kama ataweza kukutana na mwanaume muoga kama kibopa.

                                          *****

Jackson luther mpelelezi anaye sifika kwa kazi yake nzuri akaanza kupandisha ngazi kwenda juu alipo anna kwa lengo la kumtia nguvuni kwa kosa la mauaji.Anna akaanza kukimbia akipandisha ngazi kwa kasi hadi akafika alipo waacha wezake.
“tuondokeni kimenuka”

Wakasaidiana kumkokota fety ambaye amechoka sana kwa kazi ya kupambana na karim pamoja na shamsa.Wakaingia ndani ya lifti na kushuka hadi gorofa ya kwanza,jackson akaitoa bastola yeka na kuwa makini zaidi,taratibu akaanza kuuunguza mwili wa muntar na kuhakikisha kwamba uhai wa mwili huo umesharudi kwa Mungu baba.

Kitu ambacho kinamchanganya jackson luther ni juu ya nani aliyeweza kumuua karim kwani ni miongoni mwa majambazi ambao alijaribu kuwafuatilia kwa kipindi kirefu pasipo kupata mafanikio ya aina yoyote katika kazi ya uchunguzi wake.Akapandisha hadi gorofa ya tano alipomuona anna akimalizikia na akakuta korido ikiwa haina mtu hata mmoja.

Akachunguza sehemu yote na kumkuta mtu aliye anguka chini akiugulia maumivu na mlango wa kuingilia chumbani kwake ukiwa upo wazi, akamsogelea na kumpa mkono na kumuinua kutoka alipokuwa.

“umepatwa na nini?”
“kuna wadada bwana hapa,walikuwa wakipigana na kuniangusha”
“umeumia?”
“ndio nimepiga kiuno chini.”
“wameelekea wapi?”
“hata sijui wametoka vipi humu ndani kwangu”
“sawa”

Anna,fetty na halima wakaingia kwenye jiko kuu la kupikia vyakula kwa kutumia mlango wa chini wakashuka kwenye ngazi na kutokezea upande wenye maswimcming pool katika hotel,wakawatizama watu waliomo ndani ya hotel na kuona hakuna anayewatilia mashaka kwa mwendo wa umakini wakaanza kuelekea kwenye sehemu lilipo gati la kuingilia hotelini.Kabla ya kutoka nje ya geti walinzi wakawasimamisha,kwa jicho la kuiba fetty kwa kupitia kioo cha dirisha la kijumba cha walinzi akaona video inayomuonyesha akipambana na shamsa kupitia kwenye tv ndogo iliyopo kwenye kijumba cha walinzi


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )