Thursday, September 22, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 51 & 52 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia...
Nikafanya kama dorecy anavyo niagiza, gafla tukaiona gari moja mbele yetu, aina ya pick up ikiwa na watu wenye bunduki zao huku mmoja wao akiwa ameshika bomo aina ya rocket ambalo upigaji wake analiweka begani na kulifyatulia.Sote tukafunga breki za magari yetu na majamaa wakaanza kushuka huku mwenye bomo akiwa ametuelekezea kwetu akijiandaa kutufyatulia

Endelea....
Macho yangu yangu yakawatazama jamaa walio shika bunduki mikononi mwao, wote wanaonekana wapo makini katika kutushambuli sisi.Kwa kupitia kioo pembeni, nikaangalia nyuma na kuona kuna kona ambayo ipo karibu na sehemu tulipo simama, nikakanyaga mafuta na gari kuanza kuirudisha nyuma kwa kasi kubwa, jamaa wakaana kutushambulia kwa risasi ambazo kwa bahati nzuri hazikuingia kwenye gari, kitendo cha kukunja tu, bomu alilo lifyatua jamaa likapita mita chache kutoka sehemu gari letu lilipo na kwenda kugongwa kwenye miamba na kusababisha mlipuko mkubwa na mawe yakaziba barabara kwa nyuma na kushindwa kurudi nyuma.

Nikafunga breki na kulisimisha gari, sote tuakashuka kwenye gari huku bastola zetu zikiwa mikononi,tukaifungua milango ya gari na kujificha nyuma ya milango kwani uzuri wake haipitishi risasi.Bastola zetu zikawa zimeelekea kwenye kona ambapo tunatarajia majambazi kutokea.Ukimya wa kama dakika tatu ukatawala, hatukuona watu ambao wanajitokeza kwenye kona, nikataka kunyanyuka
“eddy kaa chini”

Dorecy alizungumza kwa sauti ya ukali, nikatii kwa haraka na risasi ikapiga kwenye kioo cha gari katika mlango ambao nipo mimi.Dorecy akaanza kufyatua risasi zilizo elekea walipo majambazi, kila risasi ambayo ninaipiga mimi haikumpata mtu yoyote zaidi ya kupiga pembeni, hata kama mtu nimemlenga vizuri ila haikumpata

“nakosea wapi?”
Nilizungumza kwa sauti ya juu
“kaza mkono”
Dorecy alizungumza, huku akiendelea kufyatua risasi kwa majambazi ambao wanatoa vilio vya maumivu kila aliye pigwa na risasi.Nikaingia ndani ya mlango na kuufunga mlango wa upande ambao nipo
“unafanya nini?”
“ngoja nikuonyeshe”

Nikaiwasha gari na screen(kioo), kilichopo pembeni yangu kikawaka na kuniandikia maneno yaiyo nichosha
‘system weapon empty’ ikimaanisha hakuna silaha yoyote inayoweza kufanya kazi kwani zimeisha.
“shitiii”
Nilizungumza huku nikiupiga mskani kwa kitako cha bastola
“vipi?”
“kuna, ishu nilikuwa ninaicheki kwenye hii gari.Imeisha”
“ni nini?”
“silaha, naomba hilo jaketi lako la kuzuia risasi”

Dorecy alinitazama kwa muda kisha akavua bullet proof yake na kunirushia upande niliopo,  nilalivaa vizuri na mara nyingi nilikuwa nikimuona mzee godwin akilivaa jinsi nilivyo livaa nikiwa mtoto mdogo.Kwani kuna siku nyumbani tulivamiwa na majambazia nyumbani, akatuvalisha sote kisha yeye alielekea kupambana nao na siri moja aliyo niambia ni kwamba jaketi hili linamionzi ambayo hata ukiwa umelengwa kupigwa risasi ya kichwa basi inaivuta na kukimbilia kifuani.
“vipi huku, mbele mimi ngoja nipande hapo juu”

Nilimuambia dorecy, nikapanda kwenye gemo ambalo lipo pembeni yetu, nikapanda hadi pasipo majambazi kuniona, nikatafuta sehemu nzuri ya kusimama ambayo nikawa ninawaona kwa chini, nikawahesabu kwa haraka na kuwaona wakiwa wamebaki wanne wamejibanza kwenye gari lao wakimsubiria dorecy kujitokeza, dorecy naye akawa amejibanza kwenye gari akiwasubiri wajitokeze

Nikaishika bastola vizuri, nikafumba jicho langu moja huku nikiitazama sehemu yenye mfuniko wa tanki la mafuta kwenye gari, nikameza mate mengi kisha nikafyatua risasi tatu mfululizo huku nikiwa nimeikaza mikono yangu, risasi mbili zikapiga pembeni, jambo lililo wachanganya jamaa.Risasi ya tatu ikapiga kwenye tanki la mafuta na kulifanya gari kulipuka, huku likinyanyuliwa juu na jamaa wote wakarushwa pembeni.Hadi gari linatua chini milango na matairi yake yalichanguka vibaya.

Nikashuka kwenye gemo kupitia njia niliyo pandia na kumkuta dorecy akiwa bado ameshika bastola yake akiielekezea walipo majambazi, nikatembea kwa mwendo wa tahadhari hadi ilipo gari ya majambazi, nikaanza kuhakikisha jambazi mmoja baada ya mwengine kama amekufa, ambaye ninamkuta kwenye hatua za mwisho za maisha yake nilampiga risasi ya kumsindikiza kuzimu

Nikageuka nyuma na kumkuta dorecy akiwa ananitazama kwa macho ya mshangao, kwani haamini kama nitaweza kuwapiga risasi wezake ambao amewasaliti, nikarudi lilipo gari na kuingia, nikaliwasha hadi sehemu alipo, akafungua mlango na kuingia.Nilalipitisha pembeni gari langu taratibu kulikwepa gari linalo teketea na kuandelea na safari.Dorecy akaendelea kunielekeza njia hadi tukatokea barabara inayotokea tanga kuelekea moshi

“eddy, ulisha wahi kuua?” dorecy aliniuliza
“swali gani sasa hilo?”
“hapana, kwa mtu ambaye hazifanyi hizi kazi hawezi kuwa kufanya kama ulivyo fanya wewe”
“nimefanyaje?”
“ulivyo wapiga wale, risasi waliokuwa wakikaribia kufa”
“kawaida”

Nilimjibu huku nikendelea kuendesha gari kwa umakini, macho yangu yote yakawa ni barabarani kuangali kama polisi wa usalama barabarani wapo au hakuna.Tukaingia kwenye motel iitwayo mombo motel iliyopo kwenye barabara ya mombo

“una pesa?”
Nilimuuliza dorecy
“ndio”
“kachukue chakula basi”
“utakula nini?”
“bufee,nyama chukua na soda za take way”

Dorecy akalivua shati lake na kubaki na vest ya kiume, akaziweka vizuri nywele zake ndefu, akaichomeka bastola yake kwenye buti la jeshi, mguu wa kulia na kushuka ndani ya gari.Kwa kupitia kioo cha pembeni nikawaona askari wa usalala barabarani, wakiingia kwenye geti la motel wakiwa na pikipiki.

Wakaisimamisha pikipiki nyuma ya gari langu na kunifanya nianze kupata wasiwasi, kwani sihitaji kumwaga damu tena katika eneo hili.Mmoja akaanza kulitazama gari langu vizuri, akaanza kulizunguka taratibu huku akilitazama kadi zake za usajili zilizo bandikwa kwenye kii cha mbele
“anataka nini huyu?”
Nilijizungumzia kimya kimya, akanionyesha ishara ya kufungua kioo cha gari langu, akanitazama kwa sekunde kadhaa

“habari yako afande?” nilianza kumsalimia
“salama, gari yako ilipata nini?”
“kivipi?”
“imebonyea  pembeni huku?”
“ilipata ajali, afande”
Nilizungumza huku mkono wangu wa kulia ukiwa umeishika bastola, huku nikiwa nimeficha pembeni ya siti yangu
“unatakiwa ukaiyooshe, kwa maana gari ya kifahari inakuwa haileti picha nzuri”

“sawa afande”
“insuarence yako nayo ipo katika siku za ukingoni”
“yote nitayafanya, nikifika ikulu”
Niliingiza swala la ikulu kwa maana askari, anahisi kama mimi ni miongoni mwa askari, hii nikutoka na bullet proof niliyo ivaa
“ahaaa, upo ikulu wewe?”
“yaaa”

“wezetu nyinyi wa ikulu muna kula kula pesa”
“tunakua pesa wapi kaka, kazi nyingi kama hizi unazo ziona”
“ila si kwa kila kazi unapata mkwanja mrefu?”
“inategemea, na kazi”
“ahaa sisi wa barabarani huku ni shida”
“shida gani?”
“ahaaa, madereva wenyewe wabishi kama nini”
“wabaneni”


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )