Thursday, September 22, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 53 & 54 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilioishia....
Nikanyanyuka na  kukifunga kibegi changu, nikatizama kwenye kioo cha computer yake, iliyopo juu ya meza yake, kilicho gawanyika katika vipande sita vya picha za video za kamera za ulinzi na kuona gari aina ya rangerover ikisimama kwa kasi  nje ya benki na wakashuka wasichana watano walio valia mavazi meusi huku wakiwa na bunduki mikonini mwao.Wakanza kuwashambulia askari huku walili wakiingia ndani ya benki na kuanza kuwashambulia askari na kuwaamrisha watu wote kulala chini.Nikamuona wakimuamrisha bwana turma kuingia kwenye chumba ambacho ndicho wanahifadhia pesa.

Endelea....
Japo ninaroho kidogo ya kikatili, ila kwa jinsi risasi zinavyo ngurumishwa nje na majambazi hawa, sikuthubutu hata kujaribu kutoka ndani ya chumba.Bastola yangu nikaishika vizuri kwa umakini huku macho yangu yakitazama kwenye kioo cha computer iliyopo juu ya meza.Nikawashuhudia wasichana wawili wakimuamrisha bwana turma kuingia ndani ya chumba ambacho ni chakuhifadhia pesa.Wakaendela kuingiza pesa kwenye mifuko yao, nikamuona msichana mwengine akiingia akiwa na bunduki.Sikusikia kitu anacho kizungumza.Nikaanza kusangaa baada yakuwaona watu wakivuliwa nguo na kupangwa mstari katika mlango wa kutokea nje
“wanataka kufanya nini hawa?”

Nilijiuliza swali ambalo jibu lake nikalipata  baada ya kuona watu wakitolewa nje wakiwa uchi pasipo kuwa na nguo hata moja kwenye miili yao.Wasichana wakajichanganya kwenye kundi kubwa la watu wanaotoka wakiwa, wanakimbia.Nikaitumia nafasi hiyo na mimi kutoka ndani ya chumba huku kibeki changu nikiwa nimekifunga vizuri na kukishika kwenye mkono wangu wa kushoto huku mkono wangu wa kulia nikiwa nimeishika bastola yangu.Nikajichanganya kwenye watu na kukimbilia lilipo gari letu,nikamkuta dorecy akiwa amejiinamia kwenye gari, nikafungua mlango wa gari na kuingia ndani

“eddy vipi huko?”
“tuondoke, sikwema huku”
Nikawasha gari na kuliingiza barabarani kwa kasi ya hali ya juu,
“eddy tunaelekea wapi?”
Dorecy aliniuliza huku akinitazama kwa macho makali, sikulijibu swali lake zaidi ya kuongeza mwendo kasi wa gari langu.Nikafika maeneo ya mataa na kukuta msongamano wa magari mengi yakiwa katika foleni
“shiitii”

Nilizungumza huku nikiitizama gari ndogo ya polisi inayokuja nyuma yangu kwa kasi, wakionekana kunifwatilia mimi.Kutokana nyuma yangu hakuna gari, nikairudisha nyuma gari yangu, na kuingia barabara ya pili inayopitwa na watembea kwa miguu, kazi yangu ikawa ni kupiga honi, huku nikiwa makini katika uendeshaji wangu.Watu wengi wakawa na kazi ya kulikwepa gari langu huku wengine wakijirusha kwenye mitaro kuepuka kifo
“eddy angalia mbelee”

Dorecy alizungumza kwa sauti kubwa, kwani kuku gari la abiria linakuja mbele yetu kwa mwendo wa kasi, kwa haraka sana nikakunja kushoto na kuzibaniza pikipiki za waendesha bodaboda zililozo pangwa barabarani wakisubiria wateja, kwa kupitia kioo cha pembeni, nikalishuhudia gari la abiria lilipoteza muelekeo na kuyakuma magari mengine na kusababisha ajali mbaya.Kwa ukubwa wa gari yangu haikuwa shida sana kuzikanyaga pikipiki mbili zilizopo mbele yangu.

Nikapata kiupenyo cha kuingia barabarani na cakumshukuru mungu, hakuna magari ya foleni ambayo yanaweza kunizuia kuendelea na safari yangu, huku nikiwaacha waendesha pikipiki wakitoa matusi mengi juu yangu
Kwa mbali nikaliona gari, walilokuja nalo majambazi likichanja mbuga barabara ya kuelekea mkoani

“wale ndio majambazi walio piga tukio benki”
Nilizungumza huku nililiinyooshea kidole gari la majambazi aina ya rangerover.
“mmmmm”
Dorecy aliguna, huku akinitazama machoni.Nikazidi kukanyaga mafuta na kuzidi kulisogelea majambazi, ambalo nalo linakwenda kwa mwendo wa kasi sana.

“eddy kuwa makini, wasije wakatushambulia”
“powa”
Sikuona gari yoyote ya polisi inayokuja nyuma yetu, nikazidi kulifukuzia gari la majambazi na gafla likakunja na kuingia porini
“eddy nyoosha tuu, tusiwafate”
“powa”
Nikaachana na gari la majambazi na kuelekea zangu barabara inayokwenda mikoa ya tanga na arusha.Kwa mbali nikawaona askari usalama barabarani wakiwa wamesimama.

“eddy punguza mwendo”
“huoni kama tutakamatwa?”
“nitazungumza nao mimi”
“dorecy”
“fanya hivyo, la sivyo itakuwa ni tatizo kubwa”
“powa”

Nikapunguza mwendo wa gari, na askari mmoja akatusimamisha, nikalisimamisha gari langu pembeni na askari huyo akaanza kuja kwa mwendo wa umakini, huku akilitazama gari langu.Nikaishika bastola yangu kwa umakini, ila dorecy akaushika mkono wangu wa kushoto ulio shika bastola

“tulia”
Dorecy alinizuia kufanya ambacho ninahaji kukifanya, kwa ishara askari akaniomba nifungua kioo cha gari upande nilio kaa mimi, nikatii kama alivyo hitaji mimi kufanya
“habari yako afande”
Jamaa alianza kunisalimia, nikaachia tabasamu pana ambalo muda wowote ninaweza kulibadilisha
“salama tuu, kaka”

“mbona gari yako, mbele kidogo imebonyea?”
“ahaaa kuna, mjinga alinibamiza kwenye mataa kule”
“ahaaa, munaelekea wapi?”
“nakwenda, tanga mara moja kuna kazi hapo tumeagizwa na rpc”
“kuna, gari tunaiwinda ya majambazi wamepiga tulio benki, ndio tupo tupo hapa, tunaisubiria”
“ipoje hiyo gari?”
Polisi akaniwasha simu yake na kunionyesha picha cha gari hilo

“nimetumiwa whatsap hii picha”
Dorecy akaitazama picha ya gari ambalo, tulikuwa tumeongozana nalo
“hii gari tumeongozana nayo”
Dorecy aliropoka na kunifanya nimgeukie na kumtazama kwa macho makali yaliyo jaa mshangao ndani yake
“imengia wapi?”
Dorecy akaanza kumuelekeza askari gari sehemu ilipo ingia, askari akawajulisha wezake na sisi tukaondoka.

“dorecy umefanya nini?”
“kwani tatizo lipo wapi?”
“sio tatizo lipo wapi, wewe inakuwaje unawachomesha watu wa watu katika ishu zao”
“sio ishu zao, kumbuka hata mimi ni askari”
“hata kama”
“sio hata kama, wewe hukuona ni watu wangapi walio uliwa nje ya benki”

“ila sijapenda hiyo tabia sawa”
“eddy, kumbuka hata wewe ni muhalifu”
“so”(sasa)
Nilimjibu dorecy kwa kifupi, huku nikiwa nimekasirika sana
“sihitaji hicho kibesi chako”
“unasemaje wewe?”
“sihitaji hicho kibesi chako cha kijinga, nitakubadilikia sasa hivi, umenielewa?”


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )