Monday, September 26, 2016

Zitto Kabwe: Serikali ya CCM ionyeshe kuwa inawajali Wananchi wake Kuliko inavyowapenda Mafisadi wa PAP.

NCHI HAINA DAWA MAHOSPITALINI, SERIKALI NA PAP WANAHAHA KUFUJA MABILIONI YA WATANZANIA

Gazeti la The Citizen limeandika Juu ya Suala la Ukosefu wa Madawa Katika Hospitali zote Nchini. Hii ni Habari Mbaya na Kuogopesha Kwa Watanzania Wote.

Sababu Kubwa ya Kukosekana Kwa Madawa kwenye Mahospitali nchi Nzima ni Serikali kukosa Fedha. Serikali imeipa Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) 32% Tu ya Fedha ambazo ilipaswa kutoa Kwa MSD. Serikali ilipaswa kutoa Shilingi Bilioni 62.5 Kwa MSD Katika Kipindi cha Mwezi Julai mpaka Septemba 30. Lakini mpaka Leo imeipa MSD Kiasi Cha Bilioni 20 tu.

Uchunguzi Umeonyesha mpaka Septemba 16 MSD walikuwa na Tembe za Vidonge vya Paracetamol 170,000 Tu Katika Bohari Yao ya Mbeya. Huku Nchi Hospitali zikiwa hazina Kabisa Tembe Hizo. Hali ikiwa Ni Hivyo Hivyo Hivyo Katika Dawa za Ukimwi (ARVs), Vifaa Tiba kwaajili ya Mama Na Mtoto, Dawa za kipindupindu nk.

Katika Wakati ambao imegundulika tumelipa Kampuni ya Kitapeli ya PAP kwenye Sakata la Escrow zaidi ya Dola Milioni 245 Sawa Na Shilingi Bilioni 530 - Kiasi hiki Cha Fedha Ni zaidi ya Mara Mbili ya Bajeti ya Shilingi Bilioni 251 ya MSD Kwa Mwaka. Na tukilipa Bilioni 320 tunazodaiwa Baada ya Hukumu ya ICSID tutakuwa tumelipa zaidi ya Mara Tatu ya Bajeti ya MSD Kwa Mwaka.

Serikali ya CCM ionyeshe kuwa inawajali Wananchi wake Kuliko inavyowapenda Mafisadi wa PAP.

Zitto Kabwe Ruyagwa
Septemba 26, 2016
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )