Tuesday, October 18, 2016

Mauzo ya hisa katika Soko la Hisa Dar (DSE) yaporomoka kwa asilimia 94

Mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yameshuka katika kipindi cha wiki iliyopita kwa 91% kutoka Tsh 32.5 Bilioni na kufikia Tsh 3 Billion. Pia Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zimeshuka kwa 94% kutoka 9 millioni hadi laki 5.

Afisa Masoko Mwandamizi wa DSE, Marry Kinabo, wakati akisungumza na waandishi wa habari jana, alisema kilichochangia kushuka kwa idadi ya mauzo ya hisa ni kutokana na wiki husika kuwa na siku pungufu za kazi na kwamba mauzo ya hisa hizo yalifanyika kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi ya tarehe 13 ambapo siku iliyofuata (Ijumaa) ilikuwa siku kuu ya kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julias Kambarage Nyerere.

Vile vile, Kinabo alisema kuwa, kutokana na idadi ya mauzo ya hisa kushuka, kumepelekea ukubwa wa mtaji wa soko hilo kushuka kwa 3% kutoka Trilioni 21.49 hadi Trilioni 20.8

Aidha, alitaja kampuni zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kuwa ni CRDB kwa 53%, TCC 41% na TBL 4%.

Hata hivyo, alisema mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kile kile cha Trilioni 8.13 wakati viashiria katika Sekta ya viwanda (IA), Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) na Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii umebaki kama awali.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )