Wednesday, October 19, 2016

NMB Kuendelea Kusherehekea Huduma Kwa Mteja Kwa Mwezi Mzima

Wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba hujulikana kama wiki ya huduma kwa mteja na huadhimishwa duniani kote. Benki ya NMB imeamua kuendelea kusherehekea huduma kwa mteja kwa mwezi mzima ili kuonyesha jinsi inavyomjali mteja kibiashara, kimaendeleo pamoja na amani kwa ujumla. NMB imejikita kwenye kutoa huduma bora zinazofikia malengo ya wateja wa ndani na nje.
 
Kutana na Meneja Mwandamizi  wa huduma kwa wateja wa NMB, Amanda Feruzi anayetuelezea maoni binafsi na ya kampuni kuhusu huduma kwa mteja na kwanini ni muhimu kuadhimisha huduma kwa mteja.

Mimi: Karibu sana Amanda, tuanze kwa kufahamu jukumu lako ni nini?
Amanda: Jukumu langu ni kutengeneza, kuratibu, kufuatilia na kupima ubora wa huduma kwenye benki

Mimi: Huduma kwa mteja inamaanisha nini kwako na kwenye benki kwa ujumla?
Amanda: Binafsi, naamini kwamba huduma kwa mteja ni kuwaheshimu na kuwajali wateja kwa kutumia weledi kufanikisha mahitaji yao. Kama shirika – huduma kwa wateja ni jambo la msingi sana hapa NMB na ndio maana kila siku tunaboresha huduma na bidhaa zetu ili kufanikisha malendo ya wateja wetu.

Mimi: Kwanini ni muhimu kuwa na wiki ya huduma kwa mteja?
Amanda: Wateja wetu (wa ndani na nje) ndiyo sababu ya sisi kuwa na mafanikio. Kwahiyo, tunasherehekea mchango wao na kuwaahidi kwamba TUNAWAJALI kwa kuwa sehemu ya mafanikio yetu.

Mimi: Ni kitu gani cha muhimu sana cha kufuata unapokuwa unamhudumia mteja?
Amanda: Kitu cha msingi sana wakati wa kumhudumia mteja ni kuhakikisha mahitaji na matarajio yake yanafikiwa. Inapotokea kwamba kwa namna moja au nyingine hatujafikia matarajio ya mteja wetu, tunachukua mrejesho na kulifanyia kazi suala hilo.

Mimi: Msemo wa “mteja ni mfalme” una ukweli kiasi gani?
Amanda: Tunaposema mteja ni mfalme, tunarudi palepale kwenye kutilia msisitizo wa kusherehekea wiki ya huduma kwa mteja. Mteja ni mfalme kwa sababu ndiye sababu ya sisi kufanikiwa na kuongeza jitihada ili kufanikisha malengo yake. Mteja anahitaji huduma bora kwenye pesa zake hivyo, ni wajibu wetu kumsikiliza kwa makini, kumwelewa na kufanikisha mahitaji yake.

Mimi: Kama huduma kwa mteja ingekuwa ni mnyama, unafikiri angekuwa ni mnyama gani na kwanini?
Amanda: Hilo ni swali zuri lakini gumu pia. Mi nafikiri ningefananisha wiki ya mteja na tembo. Tembo ni wapole na viongozi wasiotumia mabavu. Hiyo ndio sababu tembo wenzao huwaheshimu kutokana na uwezo wao wa kutatua matatizo. Hiyo ni sawa na hhuduma kwa mteja.

Mimi: Ahsante sana kwa kuzungumza nasi kuhusu huduma kwa mteja na namna mlivyojipanga kuhakikisha kwamba mnatimiza matarajio ya wateja wenu.
Amanda: Shukrani sana.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )