Tuesday, October 11, 2016

Samsung wawataka wateja wao kutupa ‘Galaxy Note 7’, zina tatizo la kulipuka kwenye chaji

Kufuatia ripoti za matukio mengi ya watumiaji wa simu za Samsung kulipukiwa na simu hizo wakati wa kuchaji, kampuni hiyo ya Kikorea hatimaye imewataka watumiaje wake kutupa toleo la ‘Galaxy Note 7’ kutokana na tatizo hilo.

Kampuni ya Samsung imetoa tamko rasmi kupitia tovuti yake ikiwataka watumiaji wa simu hizo toleo la ‘Galaxy Note 7’ duniani kote kuchukua tahadhari na kuacha kabisa kuzitumia  wakati ikiendelea na uchunguzi zaidi.

“Tunafanya kazi na Mamlaka husika kufanya uchunguzi kuhusu kuwepo kwa ripoti za matukio yanayohusu Galaxy Note7. Kwa sabababu usalama wa mteja wetu ni kipaumbele, Samsung tunawataka wauzaji wote wa simu zetu duniani kuacha mara moja kuuza Galaxy Note 7,” imeeleza taarifa rasmi ya kampuni hiyo.

Majaribio ya betri ya simu ya Samsung, Galaxy Note 7 yaliyofanywa katika maabara moja nchini Singapore yalipelekea simu hiyo kulipuka moto.

Hivi karibuni, hata hapa Tanzania, kumekuwa na ripoti za matukio ya wananchi wengi kudai kuwa wameripukiwa na simu za Sumsung walipokuwa wanachaji. 

Pia, kulikuwa na taarifa ambazo hazikuthitishwa na Mamlaka kuhusu watu kulipukiwa na simu hizo walipozipokea wakati zikiwa kwenye chaji.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )