Friday, November 11, 2016

Misiba Yasitisha Mkutano wa Bunge Mjini Dodoma Leo

Mkutano wa Tano  wa Bunge umeahirishwa kwa namna yake baada ya muhimili huo wa dola kupata misiba mikubwa miwili.

Misiba hiyo ni wa Spika Mstaafu, Samuel Sitta aliyefariki nchini Ujerumani na Mbunge wa Dimani(CCM) Hafidh Ally ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia leo (Ijumaa) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Dodoma.

Mara baada ya kutangaza  kifo cha Hafidh Spika wa Bunge,  Job Ndugai alimtaka Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Ajira, Kazi, Vijana Jenista kutengua kanuni ili  kuwezesha mambo vote kufanyika.

Spika alimtaka Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria  Ndogo Ndogo, Andrew Chenge kuhitimisha hoja yake ya taarifa ya Kamati iliyowasilishwa juzi bila kujadiliwa na wabunge ili  Serikali yaweze kufanyia kazi.

Baada ya kufanya hiyo, Spika ameahirisha bunge hadi saa  8.30 mchana kwa ajili ya kikao maalum cha Bunge.

Amesema mara  baada kikao maalum cha bunge kumuaga Sitta basi  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atatoa hoja yake kuahirisha Bunge kwa  kifupi sana  tofauti na wakati mwingine.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )