Saturday, November 5, 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 35 & 36

Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA  
“Asante sana Fred”
Wakiwa juu angani, wakaendelea kupata vinywaji mbalimbali, huku wakitazama baadhi ya chanel, za tv ndogo iliyopo kwenye kila meza ya safa lililopo ndani ya ndege hiyo ya kifahari. Gafla Rahab akaanza kujihisi vaibaya vibaya, huku mara kadhaa, akawa anajikaza ili Praygod asijue ni kitu gani kinacho endelea, ila gafla akajikuta akianza kutapika na kulichafua gauni lake alilo livaa

ENDELEA  
Furaha ikabadilika na kuwa mshike mshike ndani ya ndege kwani kadri muda ulivyo zidi kwenda hali ya Rahab ikaanza kubadilika na kujikuta mwili mzima ukianza kumtetemeka, na kutoa mapuvu mdomoni mwake. Frednando akawaamuru marubani wairudishe ndege haraka kwenye kiwanja cha nyumba kwake ili kumuwahisha Rahab, aweze kuonana na madktari.

Macho ya Rahab yakabadilika na mboni zake nyeusi zikapotea na kubaki weupe kwenye macho yake jambo lililozidi kumchanganya raisi Praygod pamoja na Frednando ambaye hakujua ni ugonjwa gani ambao bibi harusi ameweza kuupata.
Haikuchukua muda mwingi, matairi ya ndege yakawa yanaserereka kwenye ardhi ya uwanja wa nyumbani kwa Frednando, ambapo Alisha waeleza madaktari wake wawe tayari kwa kumpokea mgonjwa.

Kwa kushirikia na Frednando, wakambeba Rahab na kumtoa nje ya ndege na kumuingiza kwenye gari maalumu la wagonjwa lililokuwa likiwasubiri. Moja kwa moja Rahab akakimbizwa kwenye jingo linalo tumiwa na Fredando kama hospitali inayo mtibu yeye na familia yake pale wanapo patwa, na hali yoyote ya kuumwa. Uzuri wa eneo lilipo jumba la Frednando, aliweza kuwekeza pesa nyingi kujijengea vitu muhimu kwa mahitaji yake, ikiwemo jengo la hospitali, lenye madaktari bingwa ambao Fredinando anawaamini sana

“Kaka hivi mke wangu atapona kweli?”
Raisi Praygod alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, akamshuhudia mke wake akipakizwa kwenye kitanda cha matairi baada ya kushushwa ndani ya gari, na moja kwa moja akaingizwa kwenye chumba kilicho jaa vifaa muhimu kwa kumuhudumia mgonjwa mahututi

“Atapona tu, usijali rafiki yangu”
Fredinando alimfariji raisi Praygod, lakini yeye mwenye amechanganyikiwa kwani hakuamini kama siku kama hiyo kutajitokeza jambo kama hilo la kuhuzunisha. Wakiwa wamesimama kwenye nje ya mlango wenye kioo kikubwa, wakawashuhudia madaktari wakitumia mashine za kustulia mapigo ya moyo wakiziweka kwenye kifua cha rahabu ambaye amezima kabisa mapigo yake ya moyo.
Machozi taratibu yakaanza kumtoka raisi Praygod, hakuamini uzuri wote wa Rahab, unaweza kupotea muda wowote kuanzia sasa.

“Kaka jikaze”
Frednando alizungumza huku, naye machozi yakiwa yanamtiririka, uchungu anao upata rafiki yake, nao unaugusa moyo wake, kwani ni dakika chacha tu wametoka kucheka na kufurahi na shemeji yake ambaye muda mwingi anapenda kumtania kwa jina la ‘AFRICAN QUEEN’. Mashine zakupulia zinazo soma mapigo ya moyo jinsi yanavyo kwenda yakazidi kuwachanganya madaktari hawa wane, kwani ni mstari mmoja ulio nyooka ndio unakatiza kwenye mashine hiyo, huku kukisomeka sifuri mbili za rangi nyekundu zikiashiria kwamba Rahab mapigi ya moyo hayafanyi kazi, moja inawezekana amesha fariki au moyo wake upepata mstuko mkubwa
                                                                                           ***
Si Fetty wala mwenzake yoyote aliye weza kujinyanyua kutoka kwenye sakafu walipo kaa, kila mmoja macho yake yaliyo jaa machozi, wakawa wanaitazama sura ya kipande cha mwanaume, aliye fura kwa hasira na si mwingine bali ni bwana Rusev, aliye simama huku bastola yake ikiwa mkononi mwake. Kila mmoja akatamani kujitetea, ila nguvu hakuwa nazo za kutosha kusema anaweza kupambana na bwana Rusev, anaye onekana kuchukia baada ya mapiganaji yake matatu kuuliwa kinyama
“Hatuna tulicho kibakisha tena duniani, tumekuwa ni watu waovu. Hatuna pa kwenda zaidi ya kaburini. Tuue sisi yupo tayari”
Anna alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, huku mikono yake yenye kufungwa pingu akiendelea kumshika Halima, aliye kwenye hali ngumu sana.
“Ehee Mungu zipokee roho zetu, na utusamee makosa yetu tuliyo yafanya. Amen”

Anna alizungumza kwa sauti ya unyonge iliyo wafanya wezake kuendelea kulia kwa uchungu, kwani hakuna aliye tarajia kwamba maisha yake yatakuwa hivyo. Maneno ya Anna, yakamfanya bwana Rusev, kumwagikwa na chozi lililo washangaza askari wake waliopo nje wakiwatazama.
Bwana Rusev akawamrisha askari wake kuingia ndani na kuwechukua Fetty na wezake, ambapo akawaamrisha wavalinye vipande vya vigunia vyuesi kwenye vichwa vyao wasijue ni wapi wanapelekwa.

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )