Friday, November 25, 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 45 & 46

Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA  
Majibu ya mlinzi huyo mwenye roho ya kikatili sana, yakaustua moyo wa makamu wa raisi kwani ameamini kwamba taarifa hiyo si nzuri kwa upande wake.
“Raisi Praygod Makuya anaelekea hospitalini kuonana na Samson”
“WHAT………!!!”  
Makamu wa raisi alijikuta akiishiwa na nguvu, akajibwaga kwenye sofa lililopo karibu yake akibaki amemtumbulia mimacho mlinzi wake huyo.
                                                                                    
ENDELEA  
Makamu wa raisi akakaa kimya kwa muda akifikiria ni kitu gani anaweza kukifanya, gafla akasimama huku akitabasamu
“Bimgo”
Alizungumza huku akimuomba mlizi wake simu. Akaminya baadhi ya namba kisha  akaiweka simu yake sikioni, baada ya dakika kadhaa ikapokelewa na sauti nzito ya kiume.
“Yaa ni mimi”

Makamu wa raisi alizungumza, na kumfanya mtu aliye ipokea simu hiyo kuweza kujua anazungumza na nani.
“Kuna mgonjwa hapo hospitalini kwako, somebody Samsoni. Ninahitajia umuondoe kwenye ramani ya dunia”
“Sawa nimekuelewa muheshimiwa, uishi daiama”
“Asante”
Makamu wa raisi akakata simu huku akiwa katika tabasamu pana. Ulinzi kwenye hii hoteli yake aliyo ijenga kwa usiri mkubwa pasipo serikali ya Tanzania kuweza kuifahamu, uliendelea kuimarika kila kona huku vijana wake wanao muunga mkono wakiwa makini sana kuhakikisha kwamba hakuna mtu anaye weza kufahamu kwamba kiongozi huyo anaye tafutwa na serikali ya Tanzania yupo kwenye hoteli hii kubwa ya kitalii.
                                                                                              ***
Tayari mawasiliano yalisha fanywa kwenye hospitali ya Muhimbili, ili chumba alicho lazwa Samson kifanyiwe ulinzi wa hali ya juu. Askari wenye bunduki nzito walisha weka ulinzi eneo zima la hospitali wakihakikisha kwamba anapofika Raisi Praygod Makuya, kila jambo linakuwa kwenye mstari na hakuna tatizo la kijinga litakalo kwenda kujitokeza.

Hali ya Samson, kidogo inaleta matumaini kwa madaktari, hii ni baada ya kutolewa risasi mwlinini mwake, ambazo kwa bahati nzuri hazikuweza kuleta madhara makubwa sana kwenye mwili wake.
“Nahitaji kumcheki mgonjwa”
Daktari mkuu wa kitengo cha upasuaji aliwaambia askari wawili walio simamam mlangoni mwa chumba alichopo Samson. Mmoja wa askari akachukua kitambulisho kinacho ning’inia kwenye kifua cha daktari huyo na kulisoma jina lake, ili kudhibitisha kwamba kweli ni daktari wa hospitali hiyo, alipo jiridhisha akamruhusu daktari huyo kuingia ndani ya chumba hicho.

Dokta Maliki, akasimama pembeni ya kitanda alicho lalala Samson, anaye hemea kwa mashine maalumu za kupumulia.
“Nilazima umfe mwanaharamu wewe”
Dokta Maliki alizungumza huku akivaa gloves zake nyeupe kwenye viganja vyake, ili kutoweza kuacha alama za vidole pale atakapo fanya mauaji yale alio agizwa na Makamu wa raisi. Alipo hakikisha gloves zake zipo vizuri, akachomoa mashine iliyo wekwa kwenye kinywa cha Samson, akasababisha Samson kuanza kujitingisha tingisha taratibu, akijaribu kuipigania roho yake na umauti kwani hewa iliyokuwa inaingia kwenye mapafu yake imekatishwa.
                                                                                             ***
“Endesheni haraka”
Rahab alizungumza huku akihangaika hangaika kwenye siti aliyo kalia hadi Raisi Praygod akamshangaa kwani ni kama mtu anaye hitaji kuweza kuliwahi jambo fulani.
“Kwani vipi mke wangu?”
“Kuna tatizo fanyeni haraka”
“Wapi…!!?”

“Dereva ongeza kasi tafadhali”
“Madam sote tunakwenda kwenye mwendo mmoja nikiongeza kasi mimi naweza kusababisha ajali”
Dereva anaye waendesha alizungumza kwa ukanini wa hali ya juu kwani ndivyo sheria ya kazi yake inavyo zingatia, kwenye msafara kama huo wote huwa wanaendesha katika mwendo kasi unao fanana.
“Lakini tunakaribia kufika mke wangu”
Raisi Praygod alimtoa wasiwasi Rahab, aliye yafumba macho yake kwa haraka, kama mtu anaye jaribu kuvuta hisia ya jambo fulani. Kila alipo jaribu kuvuta hisia dhidi ya jambo linalo kwenda kumtokea Samson, akashindwa kuona ni nini kinacho kwenda kutokea.

“Pleaseeeee”
Rahab alizungumza kwa sauti ya juu huku akizidi kuyafumba macho yake kwa nguvu, hadi damu za puani zikaanza kumchuruzika taratibu, Raisi Praygod akajaribu kumshika mkono mke wake kutazama ni nini kinacho msumbua, ila akajikuta mkono wake ukisogezwa kwa nguvu na mke wake huyo hadi akabaki ameduwaa.
Rahab, akashuhudia jinsi shingo ya Samson inavyo kandamizwa kwa nguvu na mtu aliye valia mavazi meupe, baada ya muda kidogo Samson akatulia kimya, ikiashiria tayari amesha yapoteza maisha yake. Rahab akayafumbua macho yake huku akishusha pumzi taratibu, machozi ya uchungu yakaanza kumwagika usoni mwake.

“Mke wangu unatatizo gani?”
Raisi Praygod aliuliza huku akiwa na wasiwasi mkubwa, Rahab akatingisha kichwa akidai hakuna tatizo ambalo limejitokeza. Rahab akajifuta damu zilizo kuwa zikimwagika, huku akiamini kwamba safari wanayo iendea haina umuhimu tena kwao. Kwani mtu wanaye mfwata tayaria amesha uawa kinyama, na mtu amabaye hakuiona sura yake.
                                                                                                  ***
Dokta Maliki, alipo hakikisha kwamba tayari amesha muua Samson kwa kuiminya shingo yake, akarudishia kila kitu alicho kitoa kwenye mwili wa Samson, ikiwemo mashine inayo msaidia kuhema. Baada ya mashine hiyo kurudishiwa kwenye mdomo wa Samson, ikaaonyesha mstari  mwekundu ulio nyooka, ukiashiria kwamba mtu huyo tayari amesha poteza maisha. Dokta Maliki akatoka ndani ya chumba hicho.
“Hakikisheni hakuna anaye ingia humu ndani, mgonjwa anahitaji kupumizika”

Aliwaambia askari hao ambao hakuna aliye kuwa akifahamu ni kitu gani kinacho endelea, Dokta Maliki akaanza kutembea kwenye kordo ndefu kuelekea nje, na muda huu hakuhitaji kukaa tena hospitalini kwani tayari anatambua ni kitu gani alicho kifanya na endapo atajulikana kama yeye ni muuaji, basi adhabu kali itaambatana naye.
Akiwa katika eneo la maegesho ya magari, gari kadhaa zinazo ashiria zimembeba kiongozi mkubwa zikasimama, ikamlazimu kuangalia ni kiongozi gani ambaye anashuka. Mlango wa gari moja ukafunguliwa akashuka binti mmoja pamoja na jaama ambaye ni mara yake ya kwanza kuiona sura yake

“Huyu ni nani?”
Alijuliza, huku akiendelea kumtazama jamaa huyo anaye wekewa ulinzi mkubwa kama kiongozi wa nchi. Macho ya dokta Maliki yakagongana na macho ya Rahab, aliye mtazama kwa muda huku akionekana kama msichana huyo anamtambua Dokta Maliki. Raisi Praygod baada ya kumuona mke wake anamshanga sana dkatari aliye simama kwenye moja ya gari huku akiwa na funguo mkononi, ikambidi amshike mke wake mkono.

“Baby twende ndani”
Rahab akaondoka na Raisi Praygod ambaye sura yake halisi imefunikwa na sura bandia ambayo hakuitaji sura yake iweze kuonekana na mtu wa iana yoyote zaidi ya walinzi wake wanao fahamu kwamba ni yeye. Dokta Maliki akiingia ndani ya gari lake na kuondoka katika eneo la hospitali ya Muhimbili huku moyoni mwake akiwa na furaha ya kuweza kukeleza kazi ya kiongozi wake anaye mtumikia.

 

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )