Wednesday, November 23, 2016

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 93 & 94(Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
Taratibu Phidaya akasimama, akanisogelea huku machozi yakimwagika. Nikataka kumkumbatia, ila akanizuia, nisifanye hivyo.
"Phida.."
Kofi zito kutoka kwa Phidaya likatua shavuni mwangu, lililo mfanya Shamsa kustuka. Phidaya akaachia msunyo mkali na kumshika mkono Jack.
"Junio tuondoke"
Phidaya alizumgumza kwa hasira, na kuanza kuondoka na mwanaye, wakijichanganya katikati ya watu walio kusanyika hapa.

ENDELEA
   Sikuhofia kukatiza katikati ya watu, kuwafwata Phidaya na mwanagu Junio. Furaha moyoni nwangu ikawa imezaliwa upya kuiona familia yangu. Iliyo nigharimu maisha yangu katika kuitafuta hadi leo kuitia machoni kwa mara ya pili, ukiachilia siku ya kwanza Junio alivyo zaliwa mbele ya macho ya watu wengi akiwemo Shatani John na Victoria.
"Phidaya, Phidaya"
Nilimuita Phidaya niliye mkaribia, kumfiki. Akasimama na kunitazama kwa macho makali sana, yaliyo jaa hasira huku machozi yakimwagika taratibu.
"Unakwenda wapi mke wangu, kumbuka nimehangaika kwa ajili yako, nimejitolea maisha yangu kwa ajili yako na mwanangu. Kwa nini unanikasiriki, kosa langu ni nini haswa?"
Nilizungu huku machozi yakianza kunitiririka.
"Nimekua muuaji kwa ajili yako, nimefanya kila niwezalo kufanya kwa ajili yako, ila umaona yote hayana dhamani si ndio?"

"Eddy nyamaza. Nilikuomba usioe, ila kwa nini ulioa. Umeniacha nahangaika, naishi maisha ya kitumwa na mwanangu. Tumekua watu wa kubadilisha majina kwa ajili yako. T...."
"Phidaya mimi sijaoa mwanamke yoyote, nilijitoa kufa na kupona kuwakomboa nyinyi mukiwa kwenye maroli kwenda kuuzwa nchi za nje. Nimefanya kosa?"
"Eddy acha uongo, haukuwa wewe, uliye tuokoa, Umemuoa mwanamke aliye nidhalilisha na kuniita mimi malaya, mimi?"
"Phidaya, achana na hayo maneno. Njoo tukamlee Junio. Twende tukaishi kwa amani na upendo. Unatambua ni mazingira gani ulimzaa Junio, huku na mimi nikiwa kwenye tabu gani."
"Junio sio mwanao, ni mwanangu peke yangu. Junio twende zetu"
Phidaya alizungumza huku akimshika mkono Junio, na kumvuta waondoke ila Junio akagoma kwenda popote.

"Mama uliniambia mtu, akiniuliza baba yangu ni nani, nimuambie simjui. Ila Eddy ni baba yangu, mara ngapi ulikua ukimpigis simu. Anamapenzi ya dhati na sisi. Mama nimechoka kuishi maisha haya ya ukimbizi. Mpe baba nafadi yake, aonyeshe ni jinsi gani anavyo tupenda."
Japo Junio kiumri ni mdogo, ila maneno aliyo yazungumza huku akilia yakanifanya mwili wangu kusisimka. Phidaya akamtizama Junio kwa macho ya mshangao, kisha akanitazama na mimi.
Nikafungua vifungo vya shati langu, nikakivua na kumpa Shamsa anishikie.
"Majeraha yote haya, nikwaajili ya kuiokoa familia yangu. Mwili wangu haukua na dhamani juu ya kuziokoa nafsi zenu. Msikilize anacho sema mwanao. Anahitaji malezi yetu sote. Tafadhali mke wangu, rudi mikononi mwangu au unataka mwanangu aendelee kuishi maisha haya ya shida. Tazama jinsi sura yake ilivyo umuka kwa kupigemwa na wezake. Je unataka awe hivi kila siku?"

Nilizungumza kwa uchungu, huku nikipiga magoti chini, sikujali ni idadi ngapi ya wagu walio tuzunguka wakitushangaa. Junio akamshika mkono mama yake.
"Mama, unanifundisha niwe mpatanishaji kwa walio gombana. Mshike baba mkono anakupenda"
Phidaya aliendelea kulia kwa uchungu, sura yake yote ikabadilika na kuwa na uwekundu fulani, kutokana na kulia kwa uchungu sana.
"Nakuomba mama, patana na baba anakuhitaji bado"
Maneno ya Junio yakamlainisha Phidaya. Taratibu Phidaya akarudi sehemu niliyo piga magoti, na yeye akapiga magoti chini, huku akilia. Kwa nguvu akanikumbatia. Nikamvuta Junio wangu, naye nikamkumbatia huku sote machozi ya furaha yakitumwagika. Watu walio tuzunguka wakaanza kupiga makofi, yafuraha. Shamsa akabaki akinikonyeza huku akitabasamu.
"Nakupenda mume wangu"
"Nawapenda wote"
Tukaendelea kukumbatiana kwa furaha.
"Eddy muda"

Shamsa alininong'oneza baada ya kuona tunakumbatiana sana. Tukanyanyuka, nikambeba Junio wangu ambaye kwa sasa anatarajia kufikisha umri wa miaka mitano.
"Nitakufanyia sherehe kubwa siku ya kuzaliwa kwako"
Nilimuambua Junio, huku tukielekea kwenye ofisi kukamilisha taratibu zote za kuwachukua Phidaya na mwanangu, na kuwa mikononi mwangu.
"Kweli baba"
"Ndio unataka ifanyikie wapi?"
"Mama kule kwa kina yule mchezaji uliye ninunulia mpira wenye jina lake ni wapi?"
"Brazil"
"Ndio, dady nataka huko huko na mimi nikawe mchezaji mpira"
"Usijali mwanangu, unaweza kucheza mpira?"
"Ndio baba nataka niwe kama Ronaldo"
"Sawa mwanangu utakuwa, tena kabla sijasahau, huyu ni Shamsa, mdogo wangu. Kwa sasa atakuwa dada yake Junio"
"Kweli dady?"
"Yeah"
Nikambusu Junio kwenye paji la uso, jambo lililo zidisha furaha kati yetu sote wanne.

               ***
   Kitendo cha ndege kutua kwenye uwanja wa ndege nchini Brazil, likawa ni jambo la kumshukuru Mungu, sote tukafungua mikanda ya siti zetu tulizo kalia, ikiashiria kwamba safari yetu immefika mwisho. Tukatoa mabegi yetu ya nguo, katika sehemu tulipo yaweka. Tukatoka ndani ya ndege kama abiria wengine. Tukafika eneo la kukaguliwa, tukafanikiwa kupita pasipo kusumbuliwa, juu ya hati zetu za kusafiria. Tulizo zikata nchini Kenya tukisaidiwa na rafiki wa Smith, aliye tukutanisha naye kipindi tunatoka Tanzania mimi na Manka, ambaye hadi sasa sijui yupo wapi.

   Kwa msaada wa ramani tuliyo pewa na rafiki wa Smith, juu ya miji yote mikuu nchini Brazili, ikatusaidia kutufikisha kwenye hoteli tuliyo kusudua kufikia tangu tukiwa nchini Kenya. Hoteli hii inapatikana pembezoni mwa fukwe za bahari zijulikanazo kwa jina la 'Copar Carban'.x
Sehemu tuliyo chukua kwa ajili ya makazi ya wiki mbili, ina vyumba vitatu, seble, kubwa pamoja na xjiko kubwa. Kila chumba kimejimudu kwa huduma zote muhimu kama choo na bafu.
"Eddy hapa umelipia bei gani?"
Phidaya alizungumza huku akikagua kagua chumba chetu cha kulala, chenye hadhi ya nyota tano.
"Kwa siku ni dola elfu sabini"
"Mmmmm kwa chumba hiki au?"
"Kwa sehemu yote, hii"
"Kweli una pesa ya kuchezea, hii ni birthday ya mwanao mambo ni haya, Je siku ya ndoa yetu itakuaje"
"Ndio ujiulize sasa, nataka kuihakikishia dunia nzima kwamba ninakupenda mke wangu"
Phidaya akanikimbilia, nilipo simama. Akanirukia na kuning'inia kifuani kwangu. Huku miguu yake akiipitisha kiunoni mwangu na kuikutanisha nyuma.

"Wewe ni mwanaume jasiri, i wish wanaume wote wangekua kama wewe. Ninaamini furaha ingepatikana katika ndoa nyingi."
"Ni wachache wenye moyo kama wangu. Ila kikubwa nimekupata wewe na mwanangu, ninaamini furaha itarudi upya"
Phidaya hakusita kuusogeza mdomo wake, karibu na mdomo wangu. Akanitazama kwa muda, kisha kwa haraka akaanza kuunyonya mdomo wangu. Kutokana na nguvu nilizo nazo, sikuweza kutetereka, kwani fujo anazo zifanya Phidaya mdomoni mwangu, huku nikiwa nimembeba, mtu unaweza kuanguka chini.

  Nikamlaza kitandani, huku akiendelea kuninyonya lipsi zangu, mikono yangu nikaishusha kifuani mwake, na kuanza kuzichezea chuchu zake. Kwa raha anazo zipata Phidaya, akajikuta akifumba macho yake. Nikazidi kuutadhimini uzuri wa Phidaya. Hapa ndipo nilipo jilaumu, kwa nini nilikua na magubegube, Sheila na Madam Mery. Kwa kupitia kioo kikubwa, kilichopo kwenye kitanda chetu. Nikamuona Junio akiwa amesimama mlangoni huku akiwa ameshika mpira alio nunuliwa na mama yake. Mdomo wake akiwa ameulegeza akishangaa tunacho kifanya.

 Nikamuona naye Shamsa, akisimama nyuma ya Junio, wote walikua na safari ya kuingia chumbani kwetu. Shamsa akamfumba macho Junio, aliyeganda akishangaa kama mshumaa wa pasaka. Shamsa akamyanyua Junio taratibu huku akiwa amemfumba macho. Akanikonyeza, na mimi nikamuonyesha ishara ya dole gumba kwa kutumia mkono wa kulia huku mkono wa kushoto akiendelea kuchezea chuchu za Phidaya. Shamsa akatabasamu, taratibu akaurudishia mlango wetu, huku mkono alio mziba macho Junio akiutumia kuufungia mlango, na kumpa fursa Junio kushangaa vya mwisho mwisho.
"Eddy ni nini hicho?"
Phidaya aliniuliza huku akiyafumbua macho, yake kutazama kila kona ya chumba.
"Kitu gani?"
"Kilicho gusa mlango"
"Hakuna kitu bby"
Phidaya akapotezea, na kuendelea na zoezi la kuunyonya mdomo wangu. Huku kila ma}ra akihakikisha ananigusa kila kona ya mwili wangu. Tukavuana nguo tulizo zuvaa, na kubaki kama tulivyo zaliwa.

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )