Sunday, December 4, 2016

Rais Dkt Magufuli afanya uteuzi wa mabalozi Wapya 21

December 03 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa Mabalozi 15 ili kujaza nafasi zilizo wazi katika Balozi za Tanzania zilizopo katika nchi mbalimbali. 

 Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mabalozi hao wameteuliwa kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika vituo vifuatavyo;
 1. Beijing – China
 2. Paris – Ufaransa
 3. Brussels – Makao Makuu ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya
 4. Muscat – Oman
 5. Rome – Italy
 6. New Delhi – India
 7. Pretoria – Afrika ya Kusini
 8. Nairobi – Kenya
 9. Brasilia – Brazil
 10. Maputo – Msumbiji
 11. Kinshasa – Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
 12. Kampala – Uganda
 13. Abuja – Nigeria
 14. Moroni – Comoro
 15. Geneva – Umoja wa Mataifa
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Mabalozi 6 kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika Balozi mpya 6 ambazo zitafunguliwa hivi karibuni katika nchi za Algeria, Israel, Korea ya Kusini, Sudan, Qatar na Uturuki.
 
Orodha kamili ya Mabalozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
 1. Balozi Mbelwa Brighton Kairuki
 2. Balozi Samuel W. Shelukindo
 3. Balozi Joseph E. Sokoine
 4. Balozi Silima K. Haji
 5. Balozi Abdallah Kilima
 6. Balozi Baraka Luvanda
 7. Balozi Dkt. James Alex Msekela
 8. Bw. Sylvester Mwakinyuke Ambokile
 9. Pindi Chana
 10. Dkt. Emmanuel J. Nchimbi
 11. Rajab Omari Luhwavi
 12. Lut. Jenerali (Mstaafu) Paul Ignace Mella
 13. Grace Mgovano
 14. Mohamed Said Bakari
 15. Job Masima
 16.  Omar Yusuf Mzee
 17. Matilda S. Masuka
 18. Fatma M. Rajab
 19. Sylvester M. Mabumba
 20. Prof. Elizabeth Kiondo
 21. George Madafa (Uteuzi wake ulishatangazwa)
Vituo vya kazi vya mabalozi hawa 21 vitatangazwa baadaye. Mabalozi wote waliobaki katika vituo ambavyo si kati ya vituo hivi 15 vilivyotajwa wataendelea na nafasi zao za uwakilishi wa Tanzania katika vituo walivyopo.
 
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemhamisha Balozi Modest Jonathan Mero kutoka kituo chake cha sasa cha Geneva, kwenda Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (New York) ambako atakuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
 
Balozi Modest Jonathan Mero anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Tuvako M. Manongi ambaye atastaafu ifikapo tarehe 06 Desemba, 2016. 

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi Grace A. Martin kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Itifaki (Chief of Protocal) – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kuanzia leo tarehe 03 Desemba, 2016.
 
Kabla ya uteuzi huo Grace A. Martin alikuwa akikaimu nafasi hiyo. Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Balozi Peter Kallaghe kuwa Afisa Mwandamizi Mwelekezi – Mambo ya Nje katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College) 

Kabla ya uteuzi huo, Balozi Peter Kallaghe alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza hadi mwanzoni mwa mwaka huu 2016.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )