Wednesday, December 7, 2016

Video: Dereva Atiwa Mbaroni Kwa Kucheza Muziki Huku Akiendesha Gari

POLISI mkoani Singida inamshikilia dereva wa gari dogo la abiria la Super Mamuu, kwa tuhuma za kuendesha kwa mwendo wa hatari.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Mayala Towo, alimtaja dereva anayeshikiliwa kuwa ni Saidi Juma (26) mkazi wa Dodoma ambaye inadaiwa siku ya tukio alikuwa anaendesha basi aina ya Nissan Civilian lenye namba za usajili T.360 DAY huku akicheza muziki.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 4, mwaka huu, saa 11: 00 jioni katika Mji Mdogo wa Itigi wilayani Manyoni wakati mtuhumiwa akiwa na wenzake watatu, alipoendesha gari hilo kwa mwendo wa hatari kwa kucheza muziki huku akiachiana usukani na wenzake hao wakati gari hilo likiwa kwenye mwendo.
Kamanda Towo aliwataja watuhumiwa wengine ambapo pia wanashikiliwa na Polisi kuwa ni Joseph Ramadhan (27), Ezekiel Joseph (24) na Sebastian Godfrey (23) wote wakazi wa Majengo, Itigi.

Hapa chini ni video ya dereva huyo akicheza wakati anaendesha gari.

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )