Sunday, January 29, 2017

Mahakama Yapiga marufuku amri ya Rais Trump kuzuia Watu Kuingia Marekani

Mahakama moja ya New York Marekani imeridhia ombi la wanaharakati waliokwenda Mahakamani kupinga amri ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo, kupiga marufuku Wakimbizi wa Syria na raia wengine wa nchi sita za kiislamu kama Iran, Iraq, Somalia, Sudan, Libya na Yemen wasiingie Marekani.

Mahakama hiyo imeamuru wote waliozuiliwa kupitia amri hizo waachiwe ikiwa ni agizo la lililotolewa saa kadhaa baada ya kuwepo Ripoti kutoka uwanja wa ndege wa John F Kennedy New York kwamba watu kadhaa wamezuiwa kuingia Marekani wakiwemo wale ambao walikuwa wamepewa ruhusa kwenda kuishi Marekani kupitia mpango maarufu wa Green Card.

Tayari pia Raia wawili wa Iraq wameishitaki Mahakamani serikali ya Marekani baada ya kushikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa John F. Kennedy New York na kuzuiwa kuingia Marekani ambapo inaripotiwa wakati huo kuna raia wengine 10 walikua wamezuiwa kuingia Marekani muda mfupi tu baada ya ndege kutua.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )