Monday, January 23, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 21 & 22 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA  
Kwa haraka Shamsa akalichukua faili na kulifungua mbele ya askari huyo hata kabla hajaondoka. Shamsa akastuka kukuta picha ya msichana ambaye alisha wahi kumuona sehemu ila kumbukumbu zake hazikumbuki ni sehemu gani ambayo aliweza kumuona. Shamsa akajikuta akiusukuma mlango na kuingia dani ya chumba hicho. Akamkuta Madam Mery akiwa amepiga magoti, wote wakamtazama Shamsa ambaye ameingia gafla,
“Dady huyu ndio aliye muua Junio”
Eddy kusikia taarifa hiyo, akastuka, kwa haraka akalichukua faili hilo na kulifunua, kitu alicho kiona picha ya Manka pamoja na jina lake pembeni.
“MANKA……..!!!! MANKA SI ALIKUFA…….??.”
  
ENDELEA
“Manka………!!!”
Madam Mery alizungumza huku akinyanyanyuka, Eddy na Shamsa wote wakamgeukia na kumshangaa.

“Hembu nione”
Madam Mery akachukua faili alilo lishika Eddy, macho yakamzidi kumtoka huku akimtazama Manka kwenye picha,
“Unamfahamu huyo?”
Eddy aliuliza huku akimtazama Madam Mery ambaye anaonekana kuwa na wasiwasi mkubwa sana. Madam Merya akajibu kwa kutingissha kichwa akionekana kumfahamu Manka.
“Hakufa”
Madam Mery alizungumza huku akimtazama Eddy usuoni kwa macho ya wasiwasi mwingi.
“Una maana gani?”
                                                                                              ***
“Ila Eddy ni chanzo cha mume mume wangu kufa”
Manka alizungumza huku akimtazama Mzee Godwin.
“Kwani, kwani uliolewa?”
“Hapana baba, ila nilikuwa na mwanaume ambaye nilimpenda sana, na alikuwa anafanana sana na Eddy”
“Nilimpenda sana yule mwanume, nakumbuka Eddy aliamua kumpa mume wangu kazi ya kwenda kumuoa Sheila aliye kuwa ni mpenzi wake, ila haikuwa hivyo kwani siku ya harusi yao ndipo walipo vamiwa na mume wangu kutekwa na kuuawa”

Maneno ya Manka yakamkumbusha Mzee Godwin, tukio ambalo yeye ndio alikuwa ni muhusika mkuu katika kupanga mpango mzima wa kuweza kumteka Eddy kwenye harusi yake yeye pamoja na mke wake. Huku akimtumia John kuweza kukamilisha mipango yote hiyo. Ila kitu ambacho kilimchanganya Mzee Godwin ni siku alipo gundua kwamba mtu waliye weza kumuu si Eddy, ila swali lililo muumiza sana kichwani mwake kijana huyo ni nani, na ametoka wapi. Leo ndio anapata jibu kamili kwamba yeye ndio muhusika mkuu wa kifo cha mpenzi wa mwanae kipenzi Manka.

Mzee Godwin taratibu akamvuta Manka hadi kifuani mwake na kumkumbatia taratibu, akaanza kumbembeleza ili asimwagikwe na machozi.
“Hatuna jinsi ya kufanya mwangu, tambua ninatafutwa ina bidi niweze kurudi makao makuu haraka iwezekanavyo”
“Makao makuu?”

“Ndio makao makuu ya kikosi changu cha DFE(Destination of my enemies)”
“Sawa, ila kuna Madam Mery yupo wapi?”
Mzee Godwin akamtazama Tom, kisha akamgeukia Manka. Kwa jinsi macho yam zee Godwin yanavyo oenekana Manka tayari akagundua kuna kitu cha tofauti kinacho endelea baina ya Mzee Godwin na Madam Mery, ambaye alisha tambulishwa na baba yake kama mama yake mdogo.
“Kuna kazi nahitaji nikupe kabla hatujaondoka”

“Sawa baba”
“Tom, huyu ni Manka ni dada yako, kuanzia hivi sasa. Jiandaeni kwa kuondoka”
Tom na Mzee Godwin wakaingia kwenye chumba amacho kimehifadhiwa pesa nyingi, wakaanza kuvikusanya vibunda vya pesa  na kuviweka kwenye mabegi yaliyo kuwa na nguo. Manka akaanza kupitia pitai vitu ambayo vipo kwenye computer ambayo baba yake alikuwa anafwatilia baadhi ya kesi ikiwemo ya kwake, hapo ndipo akakutana na sura ya binti ambaye, anakumbuka alisha wahi kuwa rafiki yake enzi za utoto.

“Huyu si Fetty?”
Manka alijiuliza huku akiendelea kuiangali picha ya Fetty, akasoma maelezo ya msichana huyo na kukuta habari ambayo ilimshangaza sana.
“Fetty ni gaidi?”
Mzee Godwin na Tom wakamaliza kukusanya pesa hizo, kisha wakaanza kuchukua baadhi ya silaha ambazo Tom hakujua kazi yake ni nini.

“Babu hizi za kazi gani?”
“Ni kwaajili ya kujilinda unaweza kutumia?”
“Hapana, nimezoea kuona kwenye video, wakina Van dame, kina Rambo wakizitumia”
“Je unahitaji kujua kuzitumia?”
“Ndio”
Tom alijibu kwa shahuku kubwa akionekana anahitaji kufahamu kutumia bunduki, jambo lililo mfanya mzee Godwin kuachia tabasam pana. Wakatoka na kumkuta Manka akiendelea kuwa bize akisoma historia ya wasichana waliopo kundi moja na Fetty wanao sadikika kuwa chini ya mikono ya serikali ya kimarekani.

  **
       Ni usiku ulio tawala shamra shamra nyingi katika ikulu ya Marekani ijulikana Whaite house, ulinzi mkali umeimarishwa kwenye kila kona ya eneo zima la ikulu. Wageni rasmi kutoka maeneo mbali mbali ya nchi ya Marekani na hata nje ya nchi ya Marekani wameudhuria, katika sherehe ya kuzaliwa kwa raisi Markn Tosh.

“Nimefika”
Sauti ya Jaquline ilisikika kwenye sikio la Agnes kupitia kifaa, maalumu alicho kifaa kwenye sikio lake, Agnes kwa kutumia mitambo maalumu ya Satelaite, anaweza kumuona Jaquline kila sehemu anapo pita, akitumia gari ndogo ya kifahari anai ya Ferrari Spider. Kwa kutumia kadi maalumu ya mualiko waliyo ipata kwa binti mmoja anaye fanya kazi ndani ya ikulu hiyo, aliweza kuionyesha kwa walinzi wanao kagua kadi ya kila mmoja anaye katika katika eneo hilo.
Wakamtazama Jaquline kwenye computer kama ni miongoni mwa waalikwa, kwa bahati nzuri wakamkuta ni mualikwa mmoja wapo.

“Welcome miss”
“Thank you”
Baada ya kumkagua, taratibu Jaquline akanza kupiga hatua kuelekea ndani ya ukumbi, wa ikulu. Macho ya Jaquline yakakutana na macho ya Lidya, binti aliye weza kuwasaidia katika kuingia katika sherehe hiyo, huku wakiwa wamemshirikisha katika mpango wao mzima wa kumteka raisi.

Lidya ni binti wa kikorea aliye kulia Marekani tangu akiwa na umri wa miaka sita, baba yake Mr Jang Woo, aliweza kuhamishiwa kikazi nchini Marekani, kama mpelelezi kwenye kitengo cha CIA. Jambo lililo mlazimu kuweza kuhamia na binti yake Lidya, aliye mbadili jina kutoka katika Jang Woo hadi Lidya, hii ni kutokana na sababu za kimsingi alizo weza kuziona ni muhimu kwa yeye kufanya hivyo ili binti yake kuweza kuwa salama.

Lidya akiwa katika umri wa miaka kumi na mbili, baba yake aliweza kupoteza maisha kwenye shambulizi la kigaidi la kulipuliwa kwa magorofa ya kiuchumi ya Marekani yaitwayo Twin Tower, na gaidi la kimataifa Osama bin Laden. Kuanzia hapo, Lidya akaanza kulelewa chini ya uangalizi wa serikali ya kimarekani katika kikosi cha CIA(Central Intrligrnce Agency).

Katika kukua kwake, wakiwa katika mafunzo ya ujasusi nchini Russia ndipo, alipo weza kukutana na Jaquline aliye muokoa kwenye ajali ya bomu lililo tegwa kwenye gari lao na magaidi walio tumwa na bwana Rusev, Jaquline akiwa ni miongoni mwa magaidi hao, ila aliweza kufanya hivyo kutokana na kutokea kumuoenea hurua binti huyo mdogo kuangamia katika kifo hicho.

Kuanzia hapo Lidya akatokea kumpenda sana Jaquline na kumuheshimu kama dada yake.
Jaquline akajichanganya na wageni wengine, huku akifwata maelekezo kutoka kwa Agnes, aliye muacha hotelini akitumia laptop yake kuweza kuona kamera zote za ikulu hiyo zinavyo fanya kazi, hii ni baada ya kupewa namba maalumu(Code) na Lidya zinazo tumia na askari walipo chumba maalimu cha ulinzi.

“Jiweke karibu na raisi”
Agnes alimpa maelekezo Jaquline naye akafanya hivyo, muda wote watu wakiwa wanaendelea kupiga stori za hapa na pale, ndivyo jinsi Jaquline alivyo zidi kuendelea kuwasoma walinzi wote walipo kwenye ukumbi huo.

 Wakati huo huo, askari mmoja akaanza kumtilia mashaka Jaquline, kwani muda wote Jaquline yupo peke yake, hana mtu wa kuzungumza naye. Askari huyo ambaye ni miongoni mwa askari wanao mlinda raisi moja kwa moja akaelekea chumba cha ulinzi, ili kufwatilia taafa muhimu za binti huyo kwani kila mgeni aliye ingia ndani ya ukumbi huo ana taarifa muhimu zinazo julikana na ikulu, na endapo kutajitokeza tatizo lolote basi, kukamatwa kwake ni rahisi.

“Mvute karibu huyo binti”
Askari huyo alimuamuru mmoja wa mafundi mitambo waliomo kwenye chumba hicho cha ulinzi kilicho jaa computer nyingi, za kisasa na zenye uwezo wa hali ya juu katika matumizi yake.
“Tafuta taarifa muhimu za huyu binti”
Kijana huyo mwenye utaalamu wa mkubwa katika maswala ya coputer, akaanza kufanya kazi aliyo agizwa. Kila kilicho anza kufanyika, Agnes aliweza kukiona, kwenye laptop yake, jinsi askari huyo wanavyo jaribu kutafuta taarifa za Jaquline.
“Jina lake ni Livna Livba, uraia ni Senegal, ni mfanya biashara mkubwa”

Kija huyo alimjibu askari huyo, kwani Lidya yeye ndiye aliye weza kuandika taarifa hizo za uaongo na kuzituma kwenye mtandao, na endapo kutatokea kitu chochote kuhusiana na Jaquline basi iwe ni rahisi kwa yeye kuto weza kujulikana uhalisia wake halisi zaidi ya sura yake tu.
“Kuna mgeni yoyote kutoka Afrika?”
“Ngoja nicheki orodha ya wageni”
Kijana huyo anaendelea kufanya alicho agizwa. Kwa bahati nzuri akakuta jina la Livba Livna katika orodha ya wageni walio weza kuhuzuria katika sherehe hiyo”
Agnes akajikuta akishusha pumzi nyingi, baada ya kuona tukio hilo, limeweza kutatulika.

“Muheshimiwa kuna tatizo”
Kijana mwengine alimwambia askari huyo, aliye kimbilia moja kwa moja kwenye sehemu alipo kaa kijana huyo na computer yake, hapo ndipo alipo weza kuiona sura ya Agnes na akionekana yupo kwenye moja ya hoteli kubwa iliyopo karibu na ikulu hiyo.
“Securty code zimeibwa, narudia tena Securty code zimeibwa, number 99902, kuna tatizo narudia tena kuna tatizo”
Askari huyo alitoa taarifwa kwa walinzi wote waliopo katika eneo la ikulu, huku akitoka kwenye chumba hicho, kwa haraka sana.

“Kuwa makini naona kama kuna jambo linalo endelea”
Agnes alimuambia Jaquline aliye endelea kuwatazama askari waliopo katika ukumbi, akagundua baadhi ya askri wanaondoka katika ukumbi huo wakieelekea nje. Agnes akawashuhudia askari baadhi wakiingia kwenye magari na kuondoka ikulu.
“Wanakwenda wapi hawa”
Agnes alijiuliza mwenyewe pasipo kugundua kwamba tayari amesha stukiwa kwamba yupo kwenye hoteli moja iliyopo karibu na ikulu, na amejulikana kwamba yeye ndio aliye husika na mauaji ya kiongozi wao bwana Paul Henry Jr.
                                                                                                  ***
“Maana yangu huyu binti yupo hai”
Eddy akamtizama Madam Mery huku akiwa amemkazia macho makali, Eddy akakumbuka siku ambayo alirudi katika kazi ya kuwaokoa Phidaya, alipo rudia nyumbani kwa Amina, rafiki wa Manka aliye kwenda kufanya naye kazi ya kuikomba familia yake, alikuta nyumbani kwa Amina kumetulia sana, akakumbuka jinsi alivyo weza kushuka na masanduku ya pesa na kuingia nayo ndani, ndipo alipo weza kukuta michirizi mingi ya damu kwenye sakafu pamoja na ukutani, ila kabla hajagundua lolote ndipo alipo weza kuvamiwa na kikundi cha kigaidia huku, Shamsa akiwa ni miongoni mwa magaidi hao.
 
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )