Wednesday, January 25, 2017

UVCCM Yatabiri Anguko la Vyama vya Upinzani

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umesema kutokana na kushamili kwa ubabe, udikteta na ung’ang’anizi  wa madaraka ipo siku viongozi wa upinzani wataondolewa kwa nguvu na aibu.

Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, jijini Dar es salaam baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana kutathmini ushindi wa uchaguzi.

Shaka amesema kuwa watanzania wataendelea kuiamini CCM kwa mambo mengi, ikiwemo kuleta uhuru na mapinduzi, sera, uongozi na utawala, kujali na kutazama maslahi mapana kwa manufaa ya umma na pia tabia ya utii wa sheria na kuheshimu katiba bila shuruti.

“Viongozi ving’ang’anizi wa madaraka ya kisiasa ni hatari kukabidhiwa dhamana ya madaraka na dola, ikitokea bahati mbaya siku moja wakapewa dhamana hiyo, hawatapisha wengine na huo utakuwa ni mwanzo wa kutikisika misingi ya utaifa, mshikamano na amani ya nchi,”amesema Shaka.

Aidha, Shaka amesema kuwa inashangaza kuwaona viongozi wa kisiasa ,akiwemo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif wakijenga himaya ndani ya vyama vyao huku wakidaiwa kufanya ubabe katika uongozi wao.

Hata hivyo amesema kuwa ukandamizaji au kukosekana  kwa uhuru wa mawazo naDemokrasia ndani ya upinzani,ni kielelezo tosha kuwa viongozi wake huimba kinadharia dhana ya demokrasia huku wakishindwa kuonyesha kwa vitendo.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )