Friday, January 27, 2017

Video: Rais Barrow alivyowasili Gambia

Maelfu ya wananchi wa Gambia wamefurika katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo, Banjul kumlaki Rais wao, Adama Barrow wakati akiwasili nchini mwake kuiongoza nchi hiyo baada ya kuondoka madarakani kwa rais wa mda mrefu Yahya Jammeh.

Barrow aliapishwa wiki iliyopita nchini Senegal wakati viongozi walipokuwa wakimshawishi Jammeh kuondoka madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi uliompa ushindi Barrow.

Barrow ameamua kurudi nchini humo mapema baada ya Wanadiplomasia kumtaka arudi mara moja nyumbani kuepuka pengo la uongozi.

Kutokana na taarifa zinazoeleza kuwa wafuasi waovu wa Jammeh wamo miongoni mwa vikosi vya usalama nchini, maelfu kadhaa ya wanajeshi wa mataifa ya Afrika magharibi wanasalia Gambia ili kuimarisha ulinzi kwa Rais Barrow.

Barrow atakaa katika makazi yake wakati ukaguzi ukifanywa katika Ikulu kutambua hatari yoyote kufuatia kuondoka kwa Yahya Jammeh kwenda uhamishoni Guinea ya Ikweta.

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )