Friday, January 27, 2017

Waziri Mkuu: Wanaojichomeka Eneo La Mgodi Ili Wapate Fidia Hawatalipwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuna baadhi ya watu wamejipenyeza na kutaka kuiibia Serikali kupitia suala la ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaopisha miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga.

Amesema kuwa Serikali haiko tayari kuona wananchi hao wakitumika kama madaraja ya wizi kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu wanaojipenyeza ili kuiibia Serikali kwa njia hiyo.

Majaliwa amesema hayo leo Januari 26, 2017 katika ziara ya kikazi mkoani Njombe, ambapo amesema kuwa watu hao ambao hawahusiki na eneo hilo la mradi wamesababisha gharama za fidia kuwa kubwa, hivyo wataalam wanatathmini ili kubaini wahusika kabla ya kulipa.

“Tunataka wananchi wenyewe waliokuwa hapa ndiyo tuwalipe fidia yao kwa mujibu wa tathmini husika. Fidia yenu mtalipwa baada ya kuwaondoa wezi wote waliojipenyeza.

“Kuna watu wanataka kuiibia Serikali kwa mgongo wenu, hili hatutakubaliana nalo. Tupo makini vumilieni inalifanyia kazi suala letu. Hakuna haki ya mtu itakayopotea,” amesema.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )