Sunday, February 12, 2017

Askofu Gwajima Afunguka Mamo Mazito Leo Jumapili baada ya kutoka Polisi

Baada ya jana Feb. 11 Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima kuachiwa na Polisi baada ya mahojiano yaliyodumu toka Alhamisi kituo cha Polisi kati Dar es salaam kufuatia sakata la dawa za kulevya, leo February 12 2017 akiwa kwenye Ibada kanisani kwake amesimulia.

"Nilienda moja kwa moja kwa Kamanda Sirro, nikamkuta na Manji, wakasema wewe na Manji tunakwenda kuwapima kwa mkemia mkuu wa Serikali, wale watu waliokuwa wanapima walikuwa wanapima kwa uwazi kabisa, wakapima vitu vyote majibu hamna chochote.

“Waliposema twende tukapime nilikua tayari, na mimi nilisema ndani yangu hata ukiona Pombe andika umeona dawa za kulevya, nikasema mimi sina tatizo twendeni nyumbani kwangu na mkikuta hata sigara andikeni ni dawa za kulevya, wakasachi na hawakukuta kitu”

==>Msikilize hapo chini akiongea
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )