Friday, February 10, 2017

Jeshi la Polisi Dar Lamjibu Mbowe......Lasema Kama Hataripoti Polisi, Basi Litamfuata Popote Alipo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji  kumhoji.

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Amesema operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa hawataruhusu tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na wale watakaoonekana watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani taarifa imeshatolewa.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )