Wednesday, February 15, 2017

Naibu Waziri wa Afya kuweka hadharani majina ya mashoga Dar es Salaam

Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa atawaweka hadharani wanaume wote wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja (mashoga) ambao hufanya biashara hiyo kupitia mitandao ya kijamii.
 
Naibu Waziri aliyasema hao jana usiku kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo alieleza kuwa yupo katika ziara jimboni kwake na mara atakaporejea jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia Dodoma rasmi ataiweka orodha hiyo hadharani.
 
Aidha, amesema kuwa wale wote wanaodhani kuwa vita dhidi ya wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni mzaha, wataona hali itakavyokuwa kwani vita hiyo ni kubwa sana na wataishinda.
 
Kigwangalla ambaye pia ni mtaalamu wa afya alisema kuwa suala la mtu kuwa shoga si suala la kibaolojia (asili) bali ni watu tu kujiendekeza na hivyo watakahikikisha wanalikomesha.
 
Sheria ya ndoa ya Tanzania inapinga watu wa jinsia moja kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi, lakini pia ni kitu kilichozuiliwa katika vitabu vitakatifu vya dini.


Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )