Saturday, February 25, 2017

Rais Magufuli Ateua Mwenyekiti Wa Bodi Mamlaka Ya Masoko Ya Mitaji Na Dhamana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,  amemteua Dkt. John Kedi Mduma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. John Kedi Mduma umeanza tarehe 23 Februari, 2017.

Dkt. John Kedi Mduma ni Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Dkt. John Kedi Mduma anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bi. Grace Rubambey ambaye amemaliza muda wake.
***


Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )