Wednesday, February 22, 2017

Ridhiwani Kikwete ajibu shutuma ya kutajwa kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya

Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete amekanusha vikali shutuma zilizotolewa dhidi yake kuhusu kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Moja ya magazeti ya leo yamechapisha habari inayomtaja mbunge huyo kujihuisha na bishara ya dawa za kulevya ambayo imekuwa ikipigwa vita kila kona ya nchi kutokana na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Gazeti hilo limeandika kuwa, jina la Ridhiwani limetajwa katika orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya na kuwa uchunguzi utafanyika. Pia limesema mbunge huyo ametoa kauli nzito kwa hadhara.

Kiongozi huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa, hafanyi biashara hiyo haramu wala hakuwahi kufikiria kuifanya na kwamba nafsi yake i tayari kufa masikini kuliko kupata utajiri kupitia njia hiyo.

Aidha, ameeleza kuwa, anaamini kwamba uchunguzi utafanywa ili kuweza kuweka mambo sawa kwani yeye hana kitu chochote cha kuficha. 

Amesema kwamba, maneno hayo ya shutuma juu yake ni ya uongo na kwamba yametolewa na watu wasiomtakia mema na wasio na haya.


==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )