Sunday, February 12, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 29 & 30 (Destination of my enemies)

ILIPOISHIA

“Muheshimiwa kama ni ushahidi basi hiyo kazi niachie mimi, nitahakikisha nay eye tunamfanya kama tulivyo mfanya baba yake”
 
Wote watano akiwemo raisi Praygod wakajikuta wakitabasamu wakiamini mpango wao umekwenda sawa sawa, lakini yote yaliyo kuwa yakiendelea ndani ya ofisi hiyo Rahab aliweza kuyasikia, hii ni baada ya kuingiza kinasa sauti kwenye suti ya mumewe pasipo yeye kujijua wakati akiwa anamuandaa wakati wa asubihi akielekea kwenye kikao hicho na washauri wake. 

Rahab akatabasamu huku akiitazama simu yake aliyo iunganisha moja kwa moja na kinasa sauti hicho. Akaachia tabasamu na kujiapiza washauri wote wa ofisi ya mume wake ni lazima wafe kwani wanataka kuipoteza furaha yake ambayo ni Eddy Godwin.

ENDELEA
***
Taarifa ya Eddy kujiuluzu katika nafasi yake ya uwaziri wa ulinzi, iliwashangaza sana wananchi wengi wa Tanzania, kila kona ya Tanzania watu walizungumza maneno yao, wengine wakimlaumu ni kwanini amefanya hivyo. 

Baadhi ya watumishi katika jeshi, wakajikuta wakiumia mioyo yao kwa kiongozi huyo waliye tokea kumpenda kutokana na utendaji wake wa kazi na kutetea masilahi yao ambayo mara nyingi huwa yanacheleweshwa sana katika kuyapata.
 
Simu ya mzee Godwin ikaingia ujube wa video, kwa haraka akaifungua video hiyo, akaanza kuitazama jinsi Eddy anavyo jiudhuru katika nafasi ya uwaziri jambo lililo mstua sana.
 
“Baba ni nini?”
Manka alimuuliza, huku akimtazama usoni mzee Godwin
“Eddy amejiudhuru uwaziri”
“Ana maana gani ya kujiudhuru”
“Hakuna anaye fahamu”
Safari yao ikachuku masaa kadhaa hadi wakafika katika nchi ya Mexco kwenye makao makuu ya kambi yake. Wakapokelewa na John akliwa na wapambe wengine. Kama kawaida wakampa heshima Mzee Godwin ambaye ndio mmiliki wa ngome nzima. 
 
“Muheshimiwa kila kitu kipo sawa”
“Kazi nzuri nahitaji uitishe kikao sasa hivi”
“Sawa muheshimiwa”
Wote wakaingia kwenye magari ya kifahari, yaliyo wapeleka mpaka kwenye jumba kubwa la kifahari waitokea kwenye uwanja wa ndege mdigo ulipo kwenye ngome hiyo. Kikao cha dharura kikaitishwa, mzee Godwin akakutana na wanajeshi wake wengi wakiwa ni waasi katika nchi zao walizo toka, ambao idandi yao ni sawa na watu elfu hamsini.
 
Nacho ya Mzee Godwin kila anavyo watazama wanajeshi wake hao walio jipanga mitsari iliyo nyooka, moyoni mwake akajihisi nguvu ya ajabu, kwani taratibu malengo yake yanazidi kuongezeka siku hadi siku. 

Agnes na Jaquline nao ni miongoni mwa wanajeshi walio panga mtari katika kundi la wanajeshi wa kike katika kiwanja kikubwa ambacho mara kwa mara hutumika kama makutano ya wote pale kiongozi wao mkubwa anapo hitaji kuzungumza nao.
 
“Destinatio of our enemies oyeeeeeeeeeeeeee”
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti kubwa na yenye ukakamavu wa hli ya juu, wanajeshi wake wote wakitikia kwa sauti ya juu huku, wakinyoosha mikono yao ya kushoto juu huku ikiwa na kofia wanazo zivaa. Mzee Godwin akarudia tena salamu hiyo, na wanajeshi wake wakajibu kama walivyo jibu mara ya kwanza kwa sauti za juu.
“Nimerudi, sasa ni mwendo wa kuhakikisha kwamba kikosi  chetu kinakua zaidi ya hapa”
 
“Mishahara ya kila mmoja wenu kuanzia mwezi huu, itaongezeka mara mbili ya jinsi anavyo lipwa”
“Sinto hitaji uzembe kati kazi yoyote ambayo itapangwa, umakini uskivu na uwajibikiaji ndio ngao yetu”
“Kiongozi wenu nipo salama kama mulivyo sikia kwamba ninatafutwa inchioni Tanzania, ila kwa uwezo wangu ninamshukuru Mungu nipo salama”
Mzee Godwin akanyamaza kidogop huku akiwatazama wanajeshi wake jinsi walivyo simama kwa uimara wa hali ya juu.
 
“Munaweza kutawanyika na kurudi kwenye shuhuli zenu”
Wanajeshi hao wakatawanyika kila mmoja akaendelea na majukumu yake ambayo wanayafanya katiaka ngome hiyo, huku wengine wakijihusiha na utengenezaji wa madawa ya kulevya aina ya Cocein, jambo linalo ifanya ngome hiyo kuzidi kutajirika siku hadi siku, wengine kazi yao ni kufanya kazi za uhalifu, kuvamia watu matajiri, mabenki makubwa, yote ni kujitahidi kuweza kuingiza kiasi kikubwa cha pesa ili huduma zao ziweze kusonga mbele. 

Wengine kazi zao ni kutengeneza silaha za kivita zenye ubora wa hali ya juu. Wengine kutengeneza ndege za kivita pamoja na magari ambayo yana uhimara mkubwa sana katika swala zima la kupambana. 

Kusema ukweli kambi ya D.F.E imakamilika kila idara, kila mmoja aliutumia ujuzi wake katika kuhakikisha kwamba maisha yake ndani ya ngome hiyo yanakuwa ni bora zaidi ya mwanzo alipo tokea.
“General kuna wageni wawili ambao tuliweza kuwaongeza kipindi haupo”
John alizungumza mara baada ya kufika katika ofisi ya mzee Godwin
 
“Kina nani?”
John akamnong’oneza mpambe wake aende akawaite Agnes na Jaquline, akafanya hivyo. Mzee Godwin akatumia fursa hiyo kuwatambulisha Tom na Manka kwa John. Baada ya dakika chache mpambe waka akarudi akiwa ameongozana na Agnes pamoja na Jaquline. Wasimama kwa heshima mbele ya Mzee Godwin huku mikono yao ikiwa nyuma. John akaanza kuwatambulisha kisha akaanza kutoa maelezo ya jinsi walivyo weza kuwapata wasichana hao, ambao wanatafutwa na serikali ya nchini Marekani.
 
“Jisikieni huru mabinti, hapa ni kama nyumbani kwenu, chochote mutakacho kihitaji basi musisite kuzungumza nasi, mimi au huyo bwana mdogo”
 
“Asante general”
Walijibu kwa pamoja, kwa heshima kubwa pamoja na unyenyekevu, kwani tayari walisha anza kuyazoea maisha ya humu ndani.
“Mimi nina ombi”
Jaqulie alizungumza kabla Mzee Godwin hajafungua kinywa chake
 
“Ombi gani?”
“Ili kuweza kuimarisha ngome hii, nimejaribu kutazama mafunzoi yanayo tolewa kila siku, ila kuna mafunzo ya uninja ambao sote wawili tunayo, hapa hayafundishwi, naoana ni vyema tukanza kuyafundisha”
“Ahaa hilo tu nawapeni ruhusa, tena itakuwa vizuri mukianza na huyu mjukuu wangu Tom”
 
“Hata mimi baba nahitaji”
Manka alizungumza huku akitabasamu
“Sawa tena huyu munatakiwa kumpa tizi la uhakika kwa maana amekuwa mzembe sana”
“Asante muheshimiwa kwa kukubali kwako”
“Musijali munaweza kwenda”
Watu wote wakatoka ofisini na kuwaacha John na mzee Godwin kuzungumza mambo mengine ya muhimu wanayo yafahamu wao wenyewe.
 
“General madam Mery yupo wapi mbona hujarudi naye?”
“Ameungana na Eddy”
Jibu la Mzee Godwin likamstua sana Joihn na kujikuta akimtumbulia macho mzee huyo kwani anamfahamu vizuri sana Eddy, akiamua lake huwa anaamua hata liwe jambo la kuhatarisha maisha yake basi atafanya hivyo ili mradi aweze kufanikiwa. Swali la kwanza alilo jiuliza endapo Eddy atagundua kwamba yeye yupo hai itakuwaje, swali hilo halikupata jibu zaidi ya kujifajiri atajua mbele ya safari
                                                                                                   ***
“Eddy kwa nini umejuzulu?”
“Sikia Samson, katika serikali hii nina maadui wengi sana, na nikiwa katika kiti cha uongozi sinto weza kufanya kazi yangu vizuri. Nahitaji kurudi kuwa Eddy, Eddy yule niliye zoea mateso na machungu ya haya maisha”
 
“Ila huoni hivi itakuwa ni hatari sana kwako?”
“Natambu ila nikiendelea kuwa katika uongozi itakuwa ni hatari sana kwani D.F.E wananitafuta kulilo kitu chochote”
“D.F.E ndio nini?”
Swali la Samson likamfanya Eddy kumtazama Samson usoni, hapo ndipo alipo amini kwamba D.F.E bado ni chama cha siri sana na hakijajulikana kwa watu wengi ndani ya Tanzania
 
“Usijali nitakuambia”
Wakiwa ndani ya handaki, wakasikia mngurumo wa gari kusimama, ikamlazimu Samson kuanza kutoka ndani ya handaki hilo na kupanda juu, akiwa makini kutazama ni nani aliye fika katika eneo hilo. Akamkuta Rahab akiwa na mlinzi wake wa kike, wamesimama nje ya gari walilo jia, lenye namba sa usajili T288 DCS, ambayo si gari ya ikulu
 
“Karibu Madam”
“Asante Eddy yupo wapi?”
“Yupo chini huko”
“Nisubirini hapa”
Rahab akawaacha Samsonm na mlinzi wake wa kike yeye akshuka chini, ikiwa nio baada ya miaka mingi sana kupita tangu alipo ondoka ndani ya handaki hilo. Gafla akastukia ngumi nzito ilioyo mfwata, kwa wepesi wake akajikuta akiikwepa na kupita pembeni.
 
“Eddy ni mimi?”
Rahab alizungumza mara baada ya kumuona Eddy akijitokeza kwenye kona aliyo kuwa amejificha akihisi kuna uvamizi umetokea kwani hakumuona Samson kushuka sehemu walipo.
“Umefwata nini huku?”
“Eddy hata salamu”
 
“Nijibu kilicho kulete wewe huku ni nini?”
“Nimekuja kukuona mpenzi wangu”
“Rahba sinto hitaji kuwa na wewe tena, nahitaji kuishi maisha yangu. Huyo memwa wako amemteka mwanangu kisa ni wewe, huoni unazidi kuniweka mimi matatani?”
Eddy alizungumza kwa kufoka hadi Rahab akatulia tuli, akimsikiliza mwanaume huyo aliye anza kufura kwa hasira na taratibu kifua chake kikianza kujaa.
“Eddy……”
“Eddy nini, unahisi kwamba nitakuelewa kwa utakacho niambia eheee?”
“Nisikilize basi mpenzi wangu, nipo tayari kufanya chochote kwa ajili yako, ili mradi nisikupoteze wewe”
“Upo tayari eheee?”

“Ndio niambie mimi nitafanya”
“Niletee Shamsa mwanangu hapa, kisha ndio tutaendelea na mambo mengine”
“Sawa”
Rahab akajisogeza karibu na Eddy akataka kumpiga busu la mdomoni, ila Eddy akamzuia kukataa busu hilo.
“Fanya hivyo umenielewa?”
“Sawa mpenzi”
Rahab alijibu huku machozi yakimlenga lenga, akatoka ndani ya pango huku akiwa na hasira kali ni kwanini mume wake amefikia mbali hadi hatua ya kumteka binti asiye na hatia katika vita hiyo inayo endelea kimya kimya.
 
“Madam….”
Samson aliita baada ya kumuona Rahab akiwapita kwa hasira na kuingia ndani ya gari na kuubamiza mlango kwa nguvu, mlinzi wake akaingia kwenye gari na yeye, akakiweka vizuri kioo chake cha mbele kinacho muwezesha kuweza kumuangalia abiria wake wa nyuma, kwa mara ya kwanza akamshuhudia bosi wake akimwagikwa na machozi, hakuelewa ni nini kilicho mfanya atokwe na machozi.
“Muheshimiwa tunaelekea wapi?”
“Popote enmdesha gari?”

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )