Friday, February 17, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 31 & 32 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
Vyombo vyote vya habari vikarusha tukio zima, ikiwa ni habari ya dharura(breaking news). Kwa kamera moja ya muandishi wa habari aliye kuwemo ndani ya jengo hilo na kujibanza kwenye moja ya kona pasipo kuonekana, aliitegesha kuelekea moja ya tv kubwa, na mawasiliano yakaruka moja kwa moja kwenye  kituao anacho kifanyia kazi, na kwakupitia video hiyo vituo vyote vya televishion nchini Tanzania vikawa vinaonyesha tukio hilo walilo liita la kigaidi, likiongozwa na waziri mstafu bwana Eddy Godwin, jambo lililo wastua wananchi wengi na kutambua maana ya waziri huyo kujiudhuru ndio hiyo.

ENDELEA
Shamsa akasimama wima pasipo kuwa na woga wowote
“Kaa chini wewe binti, kaa chini nitakupasua ubongo wako huo”
Mmoja wa watekeaji alizungumza huku bunduki yake akiwa ameielekezea kwa Shamsa, Dulla kwa haraka akamshika mkono Shamsa na kumvutia chini.

“Shamsa unataka kufanya nini, watakuua hawa watu”
“Nahitaji kuzungumza na baba yangu Eddy”
“Wasikilize watu wenyewe hawana akili kabisa hawa”
Dulla aliendelea kulalama kwa sauti ya chini, huku akiendelea kumshikilia Shamsa asiweze kunyanyuka kutoka katika sehemu aliyo lala.
“Funga mabakuli yenu wana haramu nyinyi”
Mtekaji huyo alizungumza kwa sauti ya kufoka na kuwafanya Dulla na Shamsa kunyamaza kimya.

  ***
“Madam”
Priscar alizungunza huku alimgeukia mdama Rahab aliye keti siti ya nyuma, akamkabidhi simu ambyo kuna ujumbe wa video uliingia. Rahab akaichukua simu hiyo na kutazama video hiyo.
“Ndugu wananchi, ninaimani kwa kufanya hivi serikali na wananchi kwa ujumla mutakuwa mumenielewa nini dhamira yangu, baada ya kujiudhuru”

Rahab akajikuta akistuka baada ya kumuona ni Eddy akizungumza kwenye video hiyo akiwa amevalia mavazi meusi pamoja.
“Eddy………!!”
Rahabu hakuamini macho yake kwani sura na sauti vya mtu anaye zungumza ni Eddy mwenyewe, ila kitu ambacho kinazidi kumshangaza zaid, Eddy amemuacha kwenye kwenye handaki mbalo kipindi walipo kuwa wakifanya kazi za ujambazi walikuwa wakijificha huko yeye na wezake.

“Serikali isipo hitaji kufwata matakwa yangu basi watu wote waliomo ndani ya jengo hili wateteketea kwa kupigwa risasi hadi kufa”
Ujumbe huo wa sauti ukaishia hapo, magari kwenye foleni yakaanza kuruhusiawa huku Rahab akiwa amepoteza amani ndani ya moyo wake. Kwani hiyo ni moja ya skendo ambayo itakuwa ni ngumu sana kuweza kujisafisha mbele ya wananchi ya Watanzania.

      Raisi Praygod akaitisha kikao cha dharura kwa maofisa wote wa ngazi za juu katika jeshi. Hali ya hatari inayo endelea katika jiji la Dar es Salaam kuhusiana na kutekwa kwa jengo la kibiashara la Mlimani City, ndio mada kuu ya kuweza kuzungumziwa ni jinsi gani ya kuweza kuwaokoa mateka wote wanao sadikika kutekwa na waziri  wa ulinzi, pasipo kujua kwamba mtu aliye panga mpango huo ni miongoni mwa washauri wa raisi walio panga kufanya kazi hiyo.

Vikosi vya vitengo vyote vya jeshi kuanzia polisi, jeshi, zima moto pamoja na usala wa taifa, waliweza kutumwa katika jengo la Mlimani City kuhakikisha kwamba wanaweza kuwaokoa watu wote walio weza kutekwa ndani ya jengo hilo,

Waandishi wa habari, karibia vituo vyote vya habari nchini Tanzania wakaweka kambi katika jengo la Mlimani City kuweza kurusha habari kwa mambo ambayo yanaendelea katika eneo hilo.

Sio waandhishi pekee wa Tanzania, bali hata kutoka mashirika makubwa kama BBC, Sky news pamoja na CCN, waliweza kuweka kambi ili kuitaarifu dunia juu ya kuwepo kwa tukio hilo la ugaidi ambalo limejitokeza nchini Tanzania, huku tukio hilo walikifananisha na tukio lililo tokea nchini chini Kenya miaka kadhaa iliyo pita kwa kutekwa kwa jengo la kibiashara, ambapo ni watu wengi waliweza kutekwa na wengine waliweza kupoteza maisha yao katika shambulio hilo.

Ulinzi mkali ukazidi kuimarishwa nje ya jengo la Mlimani City, barabara inayo pita kuelekea Mwenge pamoja na Ubungo zote ziliweza kufungwa, hawakuruhusiwa watu kuweza kukatiza katika maeneo hayo.
Simu ya mezani iliyopo ndani ya chumba cha kuongozea kamera zate ndani ya jengo hilo, ikaanza kuita Briton na watu wake wote wakaitazama, kila mmoja akiwa katika hali ya kujiuliza ni nani anaye ipiga simu hiyo kwani hapakuwa na mtu aliye weza kufikiria kwa muda huo kuna simu ambayo inaweza kupigwa katika eneo hilo. Briton akajikaza na kuipokea simu hiyo, ila hakuzungumza kitu chochote.

“NYOTE MUMEKUFAAAAA”
Sauti nzito inayo kwaruza kwaruza ilisikika upende wa pili wa simu hiyo, jambo lililo muogopesha Briton na kujikuta akiutoa mkonga huo wa simu sikioni mwake na kuutazama kwa macho ya mshangao.
                                                                                                 ***
“Eddy…………!!”
Manka alijikuta akishangaa huku akitazama taarifa inayo rushwa kituo cha CNN, kuhusiana na kutekwa kwa jengo la Mlimani City.
“Ndio maana nikakuambia Eddy ni mtu hatari hafai kwenye hii jamii”

Mzee Godwin alizungumza huku akimtazama Manka machoni mwake, muda wote John alikaa kimya akiitazama taarifa hiyo kwani hakujua kwamba huo ni mchezo. Kitu kinacho muumiza kichwa zaidi ni jinsi gani ambavyo Eddy anaoeneka kuwa ni mtu hatari sana kwenye mipamgo yake kwani hadi kufikia hatua ya kuweza kuteka jengo hilo kubwa la biashara nchini Tanzania, basi amekamilika katika mipango yake, ila ukweli ni kwamba mpango huo wote mzee Godwin anaufahamu, ni njia moja ambayo inaweza kumfanya adui yake huyo kukimbia kimbia ndani ya nchi yake kama aliyo kuwa akiandamwa yeye kipindi Eddy alipo kuwa madarakani.

Katika taarifa hiyo, inayo endelea kuruka, hewani kukaonyeshwa kiongozi huyo ambaye amevalia sura inayo endana na Eddy, akiwachukua wanaume wawili alio wasimamisha mbele ya kamera pasipo huruma akawatandika risasi za kichwa, jambo lililo zidi kuwastua watu wote.
                                                                                               ***
“Eddy kuna tatizo”
Samson alimuambia Eddy aliye kuwa amesimama mbali kidogo na computer hizo mara baada ya kupiga simu ya vitisho kwa watekaji hao, kwa haraka akaelekea sehemu alipokuwa amekaa Samson, akashahudia watu wawili wakiwa wameuwa kwa kupigwa risasi kisha kiongozi wao huyo akizungumza kitu.

“Atendelea kufa mmoja baada ya mwengine”
Ujumbe huo mfupi ukazidi kuwachanganya Eddy na Samson ambao hawakujua wafanye nini kwa wakati huo, Eddy akaingia kwenye chumba alicho kuwa amelala, akachangua changua kwenye nguo zililzo wekwa bila ya mpangilio juu ya meza, akabahatika kuweka kulpata koti moja jeusi refu kuanzia chini hadi juu, ambapo lina kofia kubwa, na mtu akilivaa si rahisi kuweza kujulikana. Akalivaa, alipo ona limemtosha vizuri akatoka nje ya chumba hicho na kumuuliza Samson jinsi anavyo onekana.
“Unaonekana upo vizuri”
“Basi inatupasa kuweza kuifanya hii kazi ya kuwaokoa mamia ya watu walio weza kutekwa nyara ndani ya jengo hilo”

“Tutaifanya vipi hii kazi ikiwa, usalama umeimarishwa kila kona”
“Tutajua ni jinsi gani ya kuweza kufanya ila kwa sasa inatupasa kuweza kuondoka katika eneo hili, hakuna muda mwengine wa kuweza kupoteza”
Wakatoka na Samson na kuingia kwenye gari, safari ya kurudi jijini Dar es Salaam ikaanza, akilini mwa Eddy, akawa anafikiria ni jinsi gani anaweza kuifanya kazi hiyo ya kisiri pasipo mtu yoyote kumtambua.

Mwendo wa masaa manne wakafanikiwa kufika katika jumba lake la kifahari, ambapo hapakuwa na mlinzi wa aina yoyote anaye linda hapo, macho ya askari yote yapo kwenye jengo la Mlimani City. Wakaingia kwenye moja ya chumba cha siri cha Eddy kilichopo chini ya ardhi na chumba hicho mara nyingiu huwa anaficha silaha zake za siri za kupambana endapo kunakuwa na tatizo kubwa.

Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )