Wednesday, February 22, 2017

Wanafunzi wanne kizimbani kwa kumkashifu Rais

Wanafunzi  wanne wa Chuo Kikuu cha Kampala Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, wakikabiliwa na shitaka la kuchapisha picha zinazoonyesha Rais Dk. John Magufuli amevaa hijabu kama mwanamke wa Kislamu na kuzisambaza kwenye mtandao wa WhatsApp.

Shtaka jingine ni kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya  amii (WhatsApp) kwa lengo la kumuudhi Rais.

Washitakiwa hao ni Amenitha Kongo (19), Maria Tweve (20), Agnes Gabriel (21) na Anne Mwansasu(21).

Walifikishwa mahakamani hapo jana   mbele ya Hakimu Mkazi, Catherine Kiyoja.

Akisoma mashitaka hayo, Wakili wa Serikali,  Florida Wenceslaus, alidai washitakiwa walitenda kosa hilo Juni 9, mwaka jana  Dar es Salaam.

Florida alidai washitakiwa kwa pamoja walitengeneza picha hizo kwa kutumia kompyuta na baadaye kuisambaza kwenye WhatsApp kwa lengo la kumuudhi Rais.

Washitakiwa walikana shitaka hilo na kurudishwa rumande kutokana na kutotimiza masharti ya dhamana.  Kesi itatajwa tena Machi 13, mwaka huu.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )