Sunday, March 12, 2017

Bashe: Sina Hofu Ya Kutimuliwa CCM


Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe amefunga mazito leo asubuhi kuhusiana na sakata la timua timua linaloendelea dhidi ya wanachama wasaliti ndani ya CCM huko Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM.

Mbunge huyo amesema hawezi kuwa na hofu ya aina yeyote kwa kuwa hana jambo baya alilolifanya ndani ya chama hicho hivyo hawezi kuteteleka na wanaotimuliwa wanachama.

“Sina hofu na timua timua ya wanachama wasaliti kwasababau naamini wamefanya maamuzi kwa kupitia mchakato ndani ya chama, kwa hiyo sina hofu kwasababu chama chetu kinaongozwa na katiba pamoja  na kanuni zilizopo unakuwa na hofu pale unahisi kuna jambo umelifanya kinyume na taratibu”-Alisema Bashe

Kwa upande mwingine Mbunge huyo amegoma kuzungumzia sakata la yeye kushikiliwa na Jeshi la Polisi hapo jana na kusema suala hilo kamuachia Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Abdurahaman Kinana.
==


Advertisement
Punguzo la Bei 20% msimu huu wa Idd.Agiza saa hii ya Automatic, na lipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaAdvertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )