Friday, March 24, 2017

CCM Yakanusha taarifa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Komrade Kinana Ataongea na waandishi leo

Tumekuwa tunapokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari, na pia kuna wengine wamefika mpaka ofisini, kuuliza au kuja kuhudhuria kikao baina yao na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana, asubuhi hii.

Napenda kuwafahamisha kwamba hata sisi wenyewe tumesoma tu tangazo hilo kwenye moja kati ya post za humu, hivyo naomba msihangaike nalo kwa sababu ni uzushi.

Katibu Mkuu mwenyewe yupo safarini nje ya nchi karibu wiki nzima hii.

Nawasilisha kwenu kwa taarifa sahihi.

Charles Charles
Idara ya Itikadi na Uenezi

Tarehe 24 Machi, 2017
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )