Monday, March 13, 2017

Gwajima Ajitosa Sakata La Vanessa Mdee...

Askofu Gwajima bado hajamsameha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.Akizungumza jana mbele ya waumini wa kanisa lake, Gwajima alisema:

"Sasa hapo ndio najiuliza, polisi na uhamiaji waseme kwanini wanasuasua na kuna makosa niliyoyataja angalau saba ya jinai wakati wengine wamelala ndani kwa kuhisiwa tu wakiwemo wanamuziki kwa mfano Vanessa Mdee.

"Amelala ndani tu alikuwa nje wakati sisi ametajwa naye ametajwa amerudi ndani leo siku ya tatu Vanessa Mdee leo yuko ndani kwa kuhisiwa tu.

"Lakini huyu mpaka tumetaja Daudi Bashite yupo katorokaje? Huyu kakimbiaje? Vanessa Mdee simfahamu wala simjui lakini alikuwa ana performing zake nje ya nchi kashikwa pale yuko ndani leo, huyu katorokaje? Kwanini wengine wako ndani na wengine wanazunguka mitaa ya South Africa wakati walitakiwa wawe hapa na wao, mbona mimi nilienda kulala tu?"

==>Msikilize Hapo Chini
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )