Friday, March 31, 2017

Jaji Mkuu Ampa Majukumu Tundu Lissu

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa  Ibrahim Juma ameutaka uongozi mpya wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kuusoma na kuuelewa mpango mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania ili umoja huo uweze kuchangia katika kuutekeleza.

Aliyasema hayo jana alipotembelewa na uongozi wa  TLS ulioongozwa na Rais wa chama hicho,   Tundu Lissu.

Alisema   ni vema kuusoma Mpango Mkakati huo  kufahamu ni wapi mahakama inatoka na wapi inapotaka kuelekea hususan  katika suala zima la maboresho ya huduma ya utoaji haki nchini.

Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania (2015/2016-2019/2010) umegawanyika katika nguzo kuu tatu ambazo ni utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali.

Nyingine ni upatikanaji na utoaji haki kwa wakati na kurejesha imani ya jamii na ushirikishwaji wa wadau na umejikita katika kuboresha huduma za utoaji haki kwa ujumla.

Naye Rais wa TLS, Tundu Lissu pamoja na mambo mengine  alieleza baadhi ya changamoto zinazowakabili mawakili nchini .

Alisema changamoto hizo ni  pamoja na baadhi ya mahakama kutokuwa na ofisi kwa ajili ya mawakili, taratibu za usajili wa mawakili, na nyingine.

Akijibu,  Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania,   Ilvin Mugeta alisema  Mahakama Kuu inaendelea kufanyia kazi changamoto zote zinazowakabili mawakili.

Mugeta alisema kingine kinachoangaliwa  ni kuona uwezekano wa taratibu za malipo kufanyika kwa elektroniki.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )