Thursday, March 30, 2017

Mahakama Kuu Yatengua Hukumu ya Mbunge Peter Lijualikali

Mbunge wa Kilombero mkoani Morogoro ataachiwa huru baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kutengua hukumu aliyekuwa amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero.

Peter Ambrose Lijualikali alihukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi mdogo mkoani humo.

Mbunge huyo alifanya kosa hilo kipindi cha uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero mwezi Machi 2016 ambapo upinzani walilalamikia uchaguzi huo kuwa ulijawa vurugu na vitisho vya polisi.

Polisi walimkamata Mbunge huyo baada ya kudaiwa kuwa alitaka kuingia katika chumba cha kupigia kura wakati yeye hakuwa na haki ya kupigakura.

Mahakama Kilombero ilimhukumu mbunge huyo kifungo cha miezi sita jela lakini leo Mahakama Kuu imetengua hukumu hiyo baada ya mbunge huyo kuto kukutwa na hatia, na hivyo mbunge huyo ataachiwa huru.

Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )