Wednesday, March 29, 2017

Mwakyembe Aimwagia Sifa Taifa Stars.....Adai Imemkaribisha Vizuri

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe ameipongeza timu ya Taifa ya Mpira wa miguu(Taifa Stars) kwa kushinda mechi zao zote mbili za kirafiki dhidi ya Botswana na Burundi.

Ameyasema hayo mapema hii leo wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma mara baada ya kukaribishwa rasmi Wizarani hapo.

Mwakyembe amesema kuwa Taifa Stars imempa ukaribisho mzuri katika Wizara hiyo kwa kumpa zawadi ya ushindi kwa michezo yote miwili iliyofanyika mwishoni mwa Juma lililopita na katikati mwa Juma hili.

“Nawapongeza sana wachezaji makocha na viongozi wa Taifa Stars kwa kujituma na kuipeperusha bendera ya Taifa kwa kushinda mechi zao zote mbili za kimataifa,”amesema Dkt Mwakyembe.

Aidha amewahimiza pia watanzania kuendelea kuiunga mkono Timu ya Taifa  ya Mpira wa miguu kwa vijana walio chini ya miaka 17 Serengeti Boys kwa kuichangia timu hiyo ili iweze kushinda nafasi ya kwenda kushindana katika kombe la dunia kwa vijana litakalofanyika mwezi Novemba mwaka huu nchini India.

Hata hivyo, amelipongeza pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Kamati ya kuhamasisha ushindi kwa Serengeti Boys iliyo chini ya Charles Hillary kuendelea kushirikiana kwa karibu na Wizara yake ili kufanikisha ushindi kwa timu hiyo
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )