Monday, March 27, 2017

Nape Nnauye: Matumizi ya Nguvu sana Hayalipi

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa twitter amempongeza Rais Magufuli kwa kutumia busara kumwachia msanii Nay wa mitego huku akienda mbali na kudai kuwa matumizi ya nguvu kubwa hayana faida yoyote.

“Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!"
Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia jana ambapo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam.Alikuwa anatuhumiwa kwa kutoa wimbo ambao unaikashifu serikali. 

Hata hivyo, Rais Magufuli kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, leo mchana alitoa agizo kwa Jeshi la Polisi  kumuchia huru msanii huyo na kutaka wimbo wake ‘Wapo’ uendelee kuchezwa  kwenye vyombo mbalimbali,Advertisement
==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )