Monday, March 27, 2017

Picha na Kauli ya Nay wa Mitego baada ya kuachiwa na polisi

Mwanamuziki Nay wa Mitego ameachiwa huru kutoka katika Kituo cha Polisi cha Kati Dar es Salaam ikiwa ni saa chache tangu Rais Dkt Magufuli aliporuhusu kuchezwa redioni kwa wimbo wake uliokuwa umefungiwa na BASATA.

Agizo hilo la Rais Magufuli limetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi habari mkoani Dodoma.

Waziri Mwakyembe alisema kuwa Rais Magufuli amesema wimbo huo ni mzuri, na kumshauri Nay wa Mitego aongezee mambo mengine kama  kuwataja watu ambao wanakwepa kodi, watumiaji wa dawa za kulevya.

Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia jana ambapo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam.

Baada ya kutoka, Nay wa Mitego amezungumza na waandishi wa habari na kuwashukuru wale wote waliojitokeza na kumsaidia kwa namna yoyote ile.

Amewashukuru Watanzania wote lakini pia wasanii waliokwenda kumuona na kumtumia jumbe za kumpa moyo, lakini pia mawakili wake waliopambana kwa muda wote kuhakikisha kuwa haki yake inakuwepo na kulindwa.

"Asante kwa wote walioamka na kuwa upande wangu, upande wa haki, walioamini kile ambacho nimekifanya nawashukuru sana". Amesema Nay wa Mitego 

Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )