Saturday, April 29, 2017

Kampuni ya Bia (TBL) yawafuta kazi wafanyakazi 100 ndani ya saa 24

Kampuni  ya Bia ya Tanzania Breweries (TBL), imepunguza watumishi wake takribani 100 ndani ya saa 24.

Kwa mujibu wa taatifa toka kwa  watumishi wa TBL,  watumishi waliopunguzwa ni wale wa kitengo cha masoko.

Mtoa taarifa mmoja kutoka kwenye duru za uongozi wa TBL ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kuwa uamuzi huo ulitekelezwa Jumatatu ya wiki hii.

Alisema sababu kuu ya kupunguza wafanyakazi hao ni kulinda uchumi wa kampuni baada ya mauzo ya bidhaa kuporomoka kwa kasi katika kipindi cha mwaka jana hadi mwaka huu.

Ofisa masoko mmoja wa kampuni hiyo ambaye hajakumbwa na panga la kupunguzwa kazi, alidokeza kwamba uamuzi huo unatokana na hali ya mauzo na uchumi wa kampuni kutokuwa rafiki.

Aliongeza kuwa uamuzi wa Serikali wa kuzuia biashara ya pombe kali zinazofungashwa kwenye mifuko ya plastiki(viroba) umeathiri kwa kiasi kikubwa soko la bidhaa yao aina ya Konyagi.

“ Wameachishwa kinyama sana, waliitwa siku ya Jumatatu na kuachishwa papo hapo(on spot), wakaambiwa wayaache magari yao na kusaini fomu ya kuondoka, miye kwa bahati nzuri  nimepona. Na hili jambo la viroba ndio limepigilia msumali wa mwisho,” alisema ofisa huyo.

Msemaji wa Kampuni ya TBL, Georgia Mutagahwa alipotafutwa kwa ajili ya uthibitisho wa taarifa hiyo, hakupokea simu kila ilipopigiwa.

Credit: Mtanzania
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )