Wednesday, April 5, 2017

Mbowe: CCM Hawawezi Kutuchagulia Viongozi Wetu

Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe amekitaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuacha kuwachagulia viongozi.

Kauli hiyo imekuja baada ya jana bunge kupiga kura za hapana kwa wagombea wa CHADEMA ambao walipaswa kuwa wawikilishi wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki na kusema wapende wasipende nafasi hizo mbili za CHADEMA zipo pale pale, huku akitangaza kuwa chama hicho kitakwenda mahakamani kudai haki.

"CHADEMA tutakwenda kuitafuta haki pengine, kama taifa tungetegemea kupata wawakilishi na tuwe tumemaliza uchaguzi huu wa kuwapata wawakilishi wetu kwenye Bunge la Afrika Mashariki, lakini ndiyo kwanza kwa matokeo haya na kwa utaratibu huu wa upindishaji wa sheria za uchaguzi, tutakwenda mahakamani, tutaitafuta haki hii mahali pengine" alisema Freeman Mbowe

Mbali na hilo kiongozi huyo amesema ni jambo lisilowezekana kwa chama kimoja kuwapangia wapinzani 
 
"Ni aibu kwa taifa kwamba chama kimoja kinataka kutafuta na kupitisha mgombea wa chama kingine cha upinzani, haiwezekani na haikubaliki, Spika amevunja kanuni za Bunge, sheria hazikuheshimiwa, ubabe umetumika lakini kwetu sisi ni sehemu ya mchakato wa demokrasia tutaendelea kuitafuta haki yetu". Alisema Mbowe

Kuhusu nafasi zao, Mbowe amesema, "Nafasi mbili za Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki wapende wasipende ni za CHADEMA, tutakaa tutashauriana, hawawezi kueleza sababu za msingi za kuwakataa wagombea wetu. Kwa sababu wagombea wetu wana sifa, lakini tunajua huu ni mkakati wa CCM , Rais anahusika, Waziri Mkuu anahusika na viongozi wao wanahusika. Wanatumia Sheria gani kutuchagulia wapinzani wawakilishi wetu katika Bunge la Afrika Mashariki?" Alihoji Mbowe. 
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )