Monday, April 3, 2017

Mwenge wa Uhuru kukimbizwa katika mikoa yote 31 kwa siku 195

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 zimezinduliwa rasmi jana katika uwanja wa Kumbukumbu Mjini Mpanda mkoani Katavi na unatarajiwa kuzunguka katika mikoa yote 31, ukipita kwenye halmashauri 195 kwa muda wa siku 195.

Katika sherehe hizo za uzinduzi, kiongozi wa mbio hizo kwa mwaka huu pia ametangazwa rasmi, ambapo atakuwa ni Amour Amad Amour kutoka mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar.

Kiongozi huyo atasaidiana na wenzake watano katika kukimbiza mwenge huo ambao ni pamoja na Bahati Mwaniguta Lugodisha (Geita), Bi Fatima Yunus Hassan (Kusini Pemba), Fredrick Joseph (Singida), Salome Obadia Mwakitalima (Katavi) na Shukran Islam Msumi (Mjini Magharibi).

Kauli mbiu ya mbio hizo kwa mwaka huu inasema "SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU'

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kwa niaba ya Rais wa serikali hiyo Dkt. Ali Mohamed Shein, ambapo katika ujumbe wake amesisitiza umuhimu wa watanzania wote kuweka nguvu zao katika kujenga taifa la viwanda

Alisema hadi sasa tangu serikali yake iingie madarakani kwa muhula wa pili tayari viwanda vitatu vya watu binafsi vimekwishajengwa visiwani Zanzibar

Balozi Seif alisema mbali na kaulimbiu ya mwaka huu kusisitiza umuhimu wa viwanda, pia mbio hizo zitakuwa zikieneza ujumbe kuhusu mapambano dhidi ya Malira, UKIMWI, Dawa za Kulevya pamoja na rushwa.

Mbio hizo zimeanzia katika wilaya ya Mpanda, na kilele chake kitakuwa ni Oktoba 14 katika mkoa wa Mjini Magharibi.

Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )