Wednesday, April 5, 2017

Rais Magufuli Aapisha Makatibu Wakuu, Mabalozi Na Kamishna Wa Tra Ikulu, Dar Es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha viongozi aliowateua kushika nyadhifa mbalimbali.

Hafla ya kuapishwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Dkt. Magufuli amemuapishwa Dkt. Leonard Douglas Akwilapo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Prof. Kitila Alexander Mkumbo ameapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Dkt. Ave Maria Emilius Semakafu ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mhe. Baraka Haran Luvanda ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

Mhe. Sylvester Mwakinyuke Ambokile ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Dkt. Ave Maria Semakafu kuwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Ikulu jijini Dar es salaam April 5,2017

Bw. Charles Edward Kichere ameapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Aidha, Viongozi hao wamekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Katibu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Waziri Yahaya Kipacha.

Akizungumza baada ya kuapishwa kwa viongozi hao, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapongeza kwa kuteuliwa kushika nyadhifa hizo na amewataka kufanya kazi kwa kutanguliza maslai ya Taifa na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

“Tutawapa ushirikiano wote mtakaouhitaji ili kufanikisha kazi zenu lakini na nyinyi msituangushe, Bw. Kichere tunakutegemea ukaimarishe ukusanyaji wa mapato pale TRA na pia ukawaambie maafisa wako na mameneja wa mikoa waache kutoa kauli za kuigombanisha Serikali na wafanyabiashara, wakusanye kodi kwa kufuata sheria na taratibu na pia wawe na lugha nzuri.
 
“Prof. Kitila Mkumbo tunategemea utaongeza msukumo kutatua matatizo ya maji, utasaidia kufanikisha kampeni ya kumtua Mama ndoo ya maji, Watanzania wapate maji safi na salama” amesema Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )