Thursday, April 27, 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 57 & 58 (Destination of my enemies)

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
“Kusema kweli, ndani ya gari hatukukuta mwili wa mtu yoyote. Hata tulipo jaribu jaribu kutazama pembeni kuona kwamba labda mtu au watu walio kuwemo ndani ya gari hilo watakuwa wameangukia pembeni hatukuweza kuwapata”
“Unasema kweli?”
“Ndio Mrs Ranjiti, siwezi kukutania”
Kidogo hata nguvu za miguu zikamjia Phidaya, akajikongoja kongoja kwenda kuchungulia kwenye korongo hilo huku akiongozana na askari huyo sehemu alipo onyeshwa gari ilipo kutwa, alijikuta akitoa macho kwani ina umbali mrefu sana.
‘Sasa kama wametoka watakuwa wapi’
Phidaya aliiuliza huku akiendelea kuchhungulia chungulia bondeni kwenye korongo hilo.

ENDELEA
   Phidaya hakuhitaji kuondoka katika eneo hilo hadi apate ripoti ya mwisho kutoka kwa Polisi kwamba kijana wake Lee Si pamoja na Shamsa hawakuwemo kwenye ajali hiyo. Hadi yanatimu majira ya saa nne usiku, baridi ikiwa kali katika eneo la eneo hilo pamoja na ukungu mwingi, ulio tanda kila mahali hapakuweza kuonekana mtui wa aina yoyote aliye kuwamo kwenye ajali hiyo. Jambo hilo kwa upande mmoja liampa matumaini makubwa sana Phidaya. Akaagana na mkuu wa polisi aliye fika katika eneo hilo kushuhudia kazi ya vijana wake. Kwa usalama na kutona ni usiku sana, Phidaya akapewa gari mbili za polisi ziweze kuongozana naye hadi takapo fika mjini, gari mmoja ikatangulia mbele, huku ikiwa na askari wawili na gari moja ikafwatia kwa nyuma nayo ikiwa na askari wawili.

Safari yao haikukumbwa na tatizo la aina yoyote hadi walipo mfikisha Phidaya kwenye jumba lake la kifahari, lenye ulinzi madhubuti. Akaagana na askari hao wakimuahidi watampatia ripoti kwa kila jambo ambalo litatokea kwa wakati wowote katika uchunguzi wanao endelea kuufanya juu ya chanzo cha ajali hiyo. Mfanyakazi wake wa ndani, akampokea koti alilo livua na kulishika mkononi, taratibu Phidaya akangoza hadi kwenye meza ya chakula na kuketi.

“Dokta hajarudi?”
Phidaya alimuliza mfanyakazi wake wa ndani baada ya kukuta hapakuwa na chakula ambacho kimeweza kuguswa.
“Hajarudi bado”
“Hembu nitolee simu kwenye hilo koti langu”
Mfanyakazi wake akafanya kama alivyo agizwa, Phidaya akaipokea simu yake hiyo, kitu cha kwanza alipo minya batani ya kuwashia mwanga kwenye simu yake hiyo aina ya Iphone 6, akakutana na sura ya Black Shadow. Kwa haraka kumbukumbu zake zikarudi kwa mgonjwa huyo.
Akakurupuka kwenye kiti kama kichaa, hata kula hakutamani tena, akatoka nje na kuingia kwenye gari lake, walinzi wa getini wakamfungulia geti na kuondoka kwa mwendo wa kasi sana akiwahi hospital;ini.
                                                                                                               ***
    Majira ya saa tano kasoro usiku, Kim akiwa amevalia mavazi ya udaktari, pamoja na kitambaa cha kijani alicho jifunga puani na kuziba mdomo, huku kikiwa kimembakisha macho tu. Akaanza kutembea kuelekea kwenye kordo inayo kupeleka kwenye litio ya kushukia kwenye chumba cha siri.
Mavazi yote aliyo yavaa aliweza kukabidhiwa na dokta Yan. Huku dokta Ranjiti aki nje kabisa ya hospitali yake gari lake akiwa amelisimamisha sehemu ambayo anaweza kuliona geti la hospitalini kwake na endapo gari ya kubebea wagonjwa litatoka, basi ataungana nalo kuhakikisha kwamba Black Shadow wanamuua na kumzika.

   Hapakuwa na nesi wala mtu aliye weza kumstukia Kim, kutokana na jinsi alivyo vaa. Anaonekana kama daktari anaye toka katika chumba cha upasuaji. Kim akashuka na lifti hadi kwenye chumba ambacho amelazwa Black Shadow, akatembea kwa tahadhari kubwa hadi kwenye chumba ambacho ameelelezwa atamkuta Black Shadow.
Macho yake yakatua kitandani ambapo alitegemea kumkuta Black Shadow ila haikuwa hivyo kwani hakuwepo, kilicho bakishwa hapo ni kitanda na mashuka pekee. Akahisi labda amekosea, akatoka na kuanza kukagua vyumba vingine viwili, hakukuta kitu zaidi ya maboksi yenye dawa tu.

“Shitii…….”
Kim alizungumza kwa hasira huku akiitoa simu yake mfukoni akampigia dokta Ranjiti, hazikupita hata sekunde tano simu ikapokelewa.
“Vipi umefanikisha?”
Lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa dokta Ranjiti mara tu alipo pokea simu ya Kim.
“Mbona hayupo mgonjwa mwenyewe”
“Uuuu….unasem…aje?”
“Hayupo nimeingia kwenye chumba mulicho niagiza nimekumta hayupo”

Dokta Ranjiti hakuonge kitu chochote zaidi ya kukaa kimya, Kim akakata simu na kumpigia dokta Yan, naye akaonekana kushangazwa na taarifa hiyo, kutokana yeye yupo ndani ya hospitali kwa haraka akashuka hadi kwenye chumba, akadhibitisha kwamba Black Shadow hayupo. Kila mmoja akili yake ikajikuta akichanganyikiwa haswa dokta Yan, kwani kwa ugonjwa alio kuwa nao Black Shadow ni vigumu sana kwa yeye kuondoka hapo hospitalini na isitoshe amemchoma sindano ya usingizi inayo chukua masaa mengi sana hadi kuisha kwake mwilini.
                                                                                                       ***
    Dokta Ranjiti, akataka kuliwasha gari lake na kwenda hospitali ila alipo liona gari la Phidaya likiingia katika geti la hospitalini, akasitisha zoezi lake la kwenda hospitalini, kwa jinsi alivyo changanyikiwa akahisi akili yake ikitaka kupasua kichwa chake, japo ndani ya gari lake kuna hewa ya kiyoyozi, ila jasho lilimtiririka usoni mwake kama mtu aliye kimbia mbio ndefu.

Phidaya akasimamisha gari lake kwenye maegesho, kwa haraka akashuka na kuanza kutembea kwa mwendo wa kasi kuelekea ndani. Hakuhihitaji kusemeshana na mfanyakazi yoyote, akili yake kwa wakati huo inamfikiria Black Shadow tu. Akiwa kwenye kordo akapishana na Kim akiwa ameifunika sura yake, hakumtilia maanani sana. Akaingia kwenye chumba chenye lifti, akashuka chini, akaanzaa kukimbia hadi kwenye chumba alicho lazwa Black Shadow.

Macho na sura yake vikabadilika, gafla baada ya kukuta kitanda kikiwa hakina mgonjwa, dura ikajaa mikunjo, macho yakamtoka. Mwendo kasi ukaisha, akajikuta akianza kutembea kwa taratibu kukifwata kitanda hicho. Dokta Yan aliweza kumuona Phidaya akiingia ndani ya chumba alilichokuwa amelazwa Black Shadow, yeye akiwa kwenye moja ya stoo, mara baada ya Kim kuondoka, aliingia kutafuta tafuta, kwani naye akili yake ilichanganyikiwa. Kwa woga wa kumuogopa Phidaya akajibanza kwenye maboksi mengi ya dawa akihofia kuonekana kwa maana kesi nzima itamuangukia yeye.

Phidaya akajikuta akiishiwa nguvu za miguu na kujikalia kitandani, hakujua alie, acheke au afanye nini kwa wakati huo, akili yake ikakosa kabisa maamuzi ya kufanya hali ya hatari ikamjaa moyoni mwake. Taratibu akajikuta akilala chali kwenye kitanda hicho na kutazama feni lililopo juu kwenye chumba hicho linavyo zunguka taratibu taratibu.
                                                                                                             ***
   Kitendo cha gari kuanza kwenda chini, kwenye makorongo, Shamsa akaona kupiga kelele haita kuwa jambo la msaada kwao, kwa haraka akajirusha kwenye siti ya mwisho alipo Sa Yoo, anaye endelea kupayuka kwa makelele. Kutokana kioo cha nyuma cha gari hilo kimepasuka kikampa upenyo mzuri wa yeye kujitoa kwa haraka, akamshika mkono Sa Yoo, akamchomoa kupitia katika upenyo huo. Lee Si alipo ona juhudi za wasichana hao zimezaa matunda na yeye bila kusubiria gari kufika chini kabisa, akafungua mlango na kujitosha nje na kuanza kubingiria kwenye majani marefu. Sa Yoo na Shamsa nao waakendelea kubingiria kwenda chini wakiporomoka kwenye majani marefu. Cha kumshukuru Mungu Shamsa akabahatika kushikilia kijimti kilicho mzuia kwenda chini, hivyo hivyo ikawa kwa Sa Yoo. Kwa umahiri wa mazoezi aliyo nayo Lee Si, akafanikiwa kujizuia kwenye moja ya jiwe.

Mlipuko wa gari hilo, uliwastua kila mmoja wao. Kila mmoja aliweza kulishuhudia gari hilo likiteketea kwa moto, kutokana na nyasi nyingi zilizo kuwepo katika eneo hilo, adui yao Kim, hakuweza kuwaona kwa urahisi akaamini kwamba wameteketea  kwa moto. Wakasubira kwa muda hadi walipo sikia mngurumo wa gari la adui yao Kim lilipo ondoka ndipo na wao walipo anza kufanya jitihada za kupandisha kilima hicho.

 Haikuwachukua muda sana, wakafanikiwa kufika juu barabarani, wakaanza kutembea kwa miguu wakirudi kutokea mjini, kwa mwendo wa dakika tano, wakafanikiwa kusimamisha gari la mizigo, wakapewa lifti iliyo wafikisha hadi mjini kabisa. Muda wote walitembea kwa kujihami wakihofia kuonekana na adui yao kwani hawakutambua kwamba ni sehemu gani anapatika. Wakaelekea katika nyumba ambayo Sa Yoo, alikuwa akiishi na bibi yake, na baada ya msiba wa bibi yake aliicha na kwenda kuishi na rafiki yake Shamsa.

Kila mmoja akaanza kutibu majeraha ya mwilini mwake, hususani Sa Yoo, yeye ndio amepata mikwaruzo mingi sana, sehemu za mikononi na migongoni.
“Shamsa hivi umejifunzia wapi mbinu zote zile?”
Sa Yoo aliuliza huku akitabasamu, Shamsa, hakumjibu kitu chochote zaidi ya kutabasamu na yeye.
“Haki ya Mungu nilijua leo nakufa, yaani ahaa wee acha tu. Ila kusema kweli asante rafiki yangu Shamsa, kwa maana ningekuwa sasa hivi sijui nipo kuzimu au laa”
“Unapaswa kuwa mwana mazoezi”
“Na kamwili haka kweli nifanye mazoezi gani mimi?”

“Ya kujilinda”
Muda wote wa mazungumzo Lee Si hakuzungumza kitu chochote, aliendelea kusikilizia maumivu ya vidonda vyake. Hata wazo la kumpigia simu bosi wake kumpa taarifa kwamba wapo salama wala halikuwepo akilini mwake, aliendelea kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyo fanikiwa kutoka kwenye ajali hiyo.
Shamsa na Sa Yoo wakaandaa chakula, majira ya saa mbili usiku wote kwa pamoja wakajumuika mezani na kuanza kula.
“Wewe unaitwa nani?”
Sa Yoo, alimuuliza Lee Si, baada ya kumuona akiwa ametawaliwa na mawazo mengi kichwani mwake hata chakula hakukila kwa furaha.

”Lee Si”
“Asante pia kwa kutusaidia”
“Nanyi asanteni”
“Mimi naitwa Sa Yoo, huyu anaitwa Shamsa”
“Lee kwa nini uliamua kuhatarisha maisha yako na kutusaidia sisi”
Shamsa alimuuliza Lee Si.
“Ilikuwa ni moja ya kazi yangu niliyo weza kupewa na bosi wangu”
“Bosi wako ndio amekupa kazi ya kuhatarisha maisha yako?”
“Hapana bosi wangu aliweza kunipa kazi ya kukulinda wewe”
“Mimi…….!!”
Shamsa  alishangaa huku wakitazamana na Sa Yoo, kisha akamtazama Lee Si kwa macho hayo hayo ya mshangao
“Ndio bosi wangu ndiye aliye niagiza”
“Anaitwa nani?”
Sa Yoo alidakia mada

“Anaitwa Madam Phidaya mke wa Mr Ranjiti”
Shamsa akastuka kidogo, kijoko alicho kuwa akikipeleka mdomoni kikiwa na chakula akajikuta akikishusha taratibu na kukirudisha kwenye sahani yake.
“Laiti kama nisinge kulinda basi leo hii mungekuwa nyote walili maiti hususani wewe Shamsa”
Sa Yoo na yeye macho yakamtoka, kwa jinsi macho yake yalivyo na ukubwa fulani na yaduara, kwa jinsi yalivyo mtoka hadi Lee Si akacheka kidogo.
“Unacheke sisi kufa?”
Sa Yoo aliuliza kwa woga
“Hapana siwacheki, ila nimecheka kwa jinsi ulivyo yatoa macho yako”
“Sa Yoo una simu hapo?”
“Sina simu si tumeacha nyumba ile kule”
“Na wewe Lee Si”

“Sina nahisi simu yangu imeteketea kwenye moto kwa maana niliiangusha ndani ya gari”
“Kwani simu unaitaka ya nini na wewe?”
“Nahitaji tumpigie mama”
“Mama……!!”
“Ndio mama, Phidaya ni mama yangu”
Lee Si, habari aliyo isikia nayo ni mpya masikioni mwake,naye akajikuta akishangaa. Taratibu picha ya mazungumzo ya dokta Ranjiti na Kim ikaanza kumjia taratibu kichwani mwake.
“Sasa naanza kupata picha”
Lee Si alizungumza huku akitingisha kichwa chake
“Picha gani?”
“Mpango wote wa wewe kuuliwa ameupanga mume wake dokta Ranjiti?”
“What……?”(Nini…….?)
“Ndio, kitu kinacho takiwa kwa sasa hivi ni wewe kuwa makini kwani maisha yako yapo hatarini”
“Eheee hanijui huyu, ameingia pabaya”
Shamsa alizungumza huku akiacha kula na kunyanyuka, akaanza kutembea kwa haraka kuelekea nje, wezake nao wakamfwata huku Sa Yoo akimuita.

“Unakwenda wapi sasa?”
“Nakwenda kuonana na huyo Rnjiti”
“Nisikilize Shamsa, peke yako huwezi kupambana na Ranjiti, ni mtu mwenye pesa sana na endapo atakuona tena atakuua”
Lee Si alizungungumza huku akimzuia Shamsa aliye jawa na hasira, hakujua ni kwa nini daktari huyo anahitaji kumuu kwani hapakuwa na jambo lolote baya alilo weza kumfanyia daktari huyo. Lee Si akafanikiwa kumzuia Shamsa na kumrudisha ndani. Wote watatu wakakaa kwenye meza moja kwa mazungumzo zaidi.

“Kwa nini anataka kuniua”
“Nilisikia akizungumza na mtu aliye mpa hii kazi, kwamba wewe unatambua siri ya Phidaya”
“Siri…..! Siri gani?”
“Sijajua, ila nahisi kuna jambo ambalo Phidaya mwenyewe anahitaji kulitambua, ndio maana akaamua kukutafuta wewe ili uweze kumueleza ukweli”
Shamsa akashusha pumzi nyingi, kila kitu anacho kisikia kwa wakati huu kinamchanganya akili yake.
“Nahitaji kuonana na mama”

“Kwa leo itakuwa ni ngumu kuonana naye, kwa maana usiku huu atakuwa yupo nyumbani kwake”
“Kwani sasa hivi ni saa ngapi?”
Sa Yoo akasimama na kuingia kwenye chumba chake, akaitazama saa ya ukutani kisha akarudi sebleni
“Ni nne na dakika tano”
“Atakuwa amesha toka hospitalini”
Lee Si alisisitiza. Kutajwa kwa hospitalini, Shamsa akamkumbuka Black Shadow wake.
“Mungu wangu……!!”
“Nini?”
“Black Shadow lazima yule dokta atamuua, si anatambua kwamba yule ni mpenzi wangu, ili kuendelea kufivha mauvo yake atamuua tu”

“Ohooo sasa itakuwaje?”
“Itabidi twende hospitalini haraka”
Wote watatu wakakubaliana kwa pamoja wakatoka nje na kukodisha taksi, iliyo wapeleka hadi hospitalini. Taksi yao ikasimama pembeni na kulipisha gari la wagonjwa linalo toka kwenye hospitali hiyo, huku Kim akiwa ndio derava wa gari hilo, cha kumshukuru Mungu hapakuwa na mtu aliye weza kulifwatilia gari hilo la wagonjwa wala Kim, kuifwatilia taksi hiyo kwani Kim moyoni mwake amejawa na hasira sana, kwani kazi yake haijakwenda kama alivyo kusudia. Gari hilo lilipo toka taksi nayo ikaruhusiwa kuingia, moja kwa moja ikaenda kusimama kwenye maegesho ya magari. Lee Si akatoa waleti yake, mfuko wa nyuma wa jinzi alilo vaa. Akampa dereva taksi kiasi anacho wadai, kisha akashuka kwenye taksi, akiwa eneo hilo akaliona gari la Phidaya likiwa kwenye maegesho yake ya kila siku.
“Madam yupo ndani, gari yake hiyo hapo”
Lee Si alizungumza huku akianza kutembea kwa hatua ndefu kuelekea ndani ya hospitali huku akifwatwa nyuma na Sa Yoo na Shamsa.

“Ohoo mjukuu wangu Lee Si mbona umeadimika siku hizi upo wapi?”
Bibi Eyna, alizungumza huku akiweka ndoo yake na ufagio wake wa kusafishia sakafu chini. Akamkumbatia Lee Si, kijana anaye mchukulia kama mjukuu wake.
“Nipo bibi, madam alinipa kazi kidogo nikawa nimebanwa banwa”
“Mbona umechubuka chubuka, alafu ni nyote watatu mumepatwa na nini?”
“Ahaa bibi nitakuambia badaye, vipi madam Phidaya yupo ofisini kwake?”
“Hapana nilimuona kwenye kordo akielekea chumba cha siri huko chini”
 

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )