Thursday, April 6, 2017

Spika Wa Bunge Job Ndugai Atoa Nafasi ya Mwisho CHADEMA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetoa nafasi ya pili na ya mwisho kwa ajili ya mchakato wa kuwapata wawakilishi wawili wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Akitoa taarifa yake bungeni leo , Spika wa Bunge hilo Job Ndugai amesema hadi sasa nafasi hizo bado ni za CHADEMA na atahakikisha haki hiyo wanaipata na kwamba Katibu wa Bunge atatoa taarifa ni lini mchakato huo utafanyika.

Katika hatua nyingine, Ndugai ametoa tahadhari kwa chama hicho kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa utaratibu wa kupatikana kwa wawakilishi wa Tanzania kupitia vyama vya upinzani, hivyo endapo wasipotumia nafasi hiyo, atatumia mamlaka aliyonayo kutangaza utaratibu mwingine ili Tanzania isikose wawakilishi katika nafasi hizo.

“Ikumbukwe kuwa maamuzi haya ya kuwatenganisha wabunge wa upinzani kwa  kuangalia vyama vyao ni maamuzi ya Spika, tukumbuke mabunge yaliyopita maspika wenzangu hawakufanya hivyo, waliwaweka wabunge wote wa upinzani kwenye kundi moja, mimi nikasema twende na demokrasia hii ya wawili, ambayo katika kufanya hivyo, mimi yuleyule,....tuendelee....... Hatuwezi kukubali nchi yetu ikose uwakilishi nchi yetu ikatekwa nyara kwa sababu fulani fulani". Amesema Ndugai

Pia Ndugai amewatoa hofu watanzania kuwa hawatakosa uwakilishi kwa kuwa anajua cha kufanya. "Tutatoa nafasi ya pili, lakini baada ya nafasi ya pili, tunajua hatua itakayofuata, nawahakikishia watanzania kwamba hawatakosa nafasi katika bunge hilo”

Katika uchaguzi uliofanyika juzi, Bunge hilo liliwachagua wajumbe 7 kati ya 9 waliohitajika, huku wagombea wawili wa CHADEMA  Ezekiah Wenje na Lawrence Masha wakikataliwa kwa kupigiwa kura za hapana.
Advertisement
tang
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )