Thursday, April 6, 2017

Utafiti Waweka Hadharani Mafanikio na Kasoro za Elimu Bure Nchini

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Haki Elimu unaonesha kuwa fedha za ruzuku kwa ajili ya elimu bure zinazopelekwa mashuleni hazizingatii idadi ya wanafunzi kama ambavyo inapaswa kuwa jambo ambalo limekuwa likiwapa wakati mgumu walimu wakuu mashuleni.

Akitoa matokeo ya utafiti kuhusu mpango wa serikali wa kutoa elimu bure Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, Bw. John Kallaghe amesema asilimia 95 ya walimu wakuu waliohojiwa walikiri kuwa fedha za ruzuku wanazopata hazitoshi na kushauri serikali ifanye jitihada za makusudi kuhakikisha inapeleka fedha hizo kwa wakati na kwa kuwashirikisha na wadau wa maendeleo.

Bw. Kallaghe amesema uchambuzi wa tafiti umeonesha kuwa baadhi ya shule zenye wanafunzi wachache zinapata fedha zaidi kuliko shule zenye wanafunzi wengi hali inayoashiria kutokuwa na mpangilio mzuri wa utoaji ruzuku hiyo.

Utafiti huo ulifanyika katika wilaya 7 zilizowakilisha kanda nchini nazo ni Korogwe Muleba Tabora M, Njombe , Mpwapwa, Kilosa na Sumbawanga, na kuonesha kuwa asilimia 93 ya fedha za ruzuku zilizotarajiwa shuleni zilifika.

Kwa upande wake mmoja wa watafiti wa ripoti hiyo Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. Richard Shukio, amesema japo sera ya elimu bila malipo imesaidia kuongezeka kwa uandikishaji wanafunzi hasa wa darasa la kwanza, serikali ichukue hatua za makusudi kushughulikia changamoto zilizopo za elimu.

==>Baadhi ya dondoo za matokeo ya utafiti huo
 1. Wakuu wa shule wanakubali kuwa elimu bure imepunguza mzigo kwa familia maskini.
 2. Elimu bure imewaongezea walimu mzigo wa kufundisha na wanataka nyongeza ya malipo kwa majukumu ya ziada.
 3. Nusu ya wazazi wamesema kwamba licha ya kuondolewa kwa ada bado wanaendelea kuchangia michango mbalimbali shuleni.
 4. Gharama anazoingia mzazi ni zaidi ya mara kumi ya kiwango cha shilingi 6,000 kwa mwanafunzi kinachotolewa na Serikali kuendesha shule.
 5. Mzazi mwenye mtoto katika shule ya sekondari ya bweni hutumia kiasi shilingi 250,000 katika mwaka wa kwanza.
 6. Asilimia 95 ya shule zilizoshiriki wamesema kiasi cha pesa kilichopelekwa hakikidhi mahaitaji ya shule
 7. Asilimia 93 ya kiasi cha fedha za ruzuku kilichotarajiwa kilifika shuleni.
 8. Elimu bure mesaidia kuondoa migogoro kati ya walimu na wazazi kwa sasa kwani watoto hawarudishwi tena nyumbani kuchukua michango
 9. Zaidi ya asilimia 80 ya washiriki wamesema kuwa elimu bure imewapunguzia wazazi mzigo wa michango ya mara kwa mara.
 10. Kufutwa kwa ada ya shule sio kigezo cha ongezeko la wanafunzi kutoka katika familia zilizotengwa na zenye mazingira magumu
 11. Wakuu wa shule wanne kati ya watano wanaamini kuwa elimu bure italeta madhara katika maendeleo ya taaluma ya mwanafunzi
 12. Mwalimu mmoja kwa kipindi cha elimu bure anafundisha wanafunzi 164 ukilinganisha na uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 99 mwaka 2015.
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )