Tuesday, May 9, 2017

AUDIO: Mchungaji akamatwa baada ya kuoa mke wa muumini wake

Mchungaji wa kanisa la huduma katika roho wilayani Karagwe, Jafece Josephat anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo baada ya kumuoa mke wa muumini wake na kuanza kuishi naye kama mke na mume akidai ameoteshwa na Mungu.

Mchungaji huyo amekamatwa jana baada ya kamati ya ulinzi na usalama na kamati ya amani na maadili  ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Godfrey Mheruka kufika kanisani hapo na kupata ukweli juu ya jambo hilo baada ya pande zote akiwemo mchungaji wa kanisa Josephat, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Domina Damian na mme wake wa mwanzo Donath Appolo kueleza ukweli jinsi walivyooteshwa mpaka hatua ya mke kuolewa.
==>Mkuu wa Wilaya Akimhoji Mchungaji
==>Mkuu wa Wilaya akimhoji mume wa huyo mwanamke
==>Huyu ndo mke wa mtu alieolewa na mchungaji

Mheruka alitoa agizo la kukamatwa kwa mchungaji huyo  kutokana na baba wa Appolo aliyenyang'anywa mke kujitokeza mbele ya kanisa hilo na kudai mahari aliyomtolea mtoto wake irudishwe kwani hawezi kuutolea mahari ukoo mwingine kwa kuwa mke ameshaolewa na mme mwingine.
 
"Kwa kuwa, mke ameacha familia yake akaja kuolewa na wewe mchungaji amezini na kwa kuwa wewe unayejiita mchungaji umeiacha familia yako ya watoto watano ukaoa mke mwingine nyote mnazini kwani kinachotenganisha ndoa ya mke na mme ni kifo lakini nyie mmejichukulia maamuzi yenu binafsi,"amesema Mheruka.
 
Mheruka amemwagiza mwangalizi wa kanisa hilo kuendelea kutoa huduma katika kanisa hilo ndani ya miezi sita huku akitafuta utaratibu wa mchungaji mwingine mwenye maadili mema na kuwa wao kama Serikali watachunguza vizuri kama kanisa hilo limesajiliwa au halijasajiliwa  ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa.

==>Msikilize hapo chini Mkuu wa Wilaya akimuhoji Mchungaji, mume wa huyo mwanamke na kisha huyo mwanamke

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )