Sunday, May 28, 2017

CHADEMA Wamkana Raila Odinga....Watangaza Kumuunga Mkono Uhuru Kenyatta

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza rasmi kumuunga mkono Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Kenya utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Msimamo huo umetolewa jana katika mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho unaofanyaki mjini Dodoma, ikiwa ni maamuzi ya Baraza hilo, na kutangazwa rasmi na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.

Akizungumzia uamuzi huo, Mbowe alisema sababu kuu ya uamuzi huo ni kugeukwa na mgombea wa muungano wa ODM Raila Odinga, ambaye chama hicho kilikuwa kikimuunga mkono mara zote.

Mbowe amesema "Kwa muda mrefu chama chetu kimekuwa kikimuunga mkono Raila Odinga achukue nafasi ya kuliongoza Taifa la Kenya. Mwaka 2015 ilipofika zamu yetu rafiki yetu Raila Odinga alitugeuka na kumuunga mkono adui yetu. Sisi kama Chama, safari hii tunamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na Umoja wa vyama vinavyounda JUBILEE".

==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )