Monday, May 15, 2017

Korea Kaskazini Yasema Kombora Jipya Lililorushwa Jana Lina Uwezo Wa Kubeba Nyuklia:

Korea Kaskazini imedai kwamba kombora la masafa marefu lililofanyiwa majaribio siku ya Jumapili ni kombora jipya linaloweza kubeba kichwa cha nyuklia.

Kombora hilo lililorushwa lilienda angani urefu wa kilomita 2,000 na kusafiri kilomita 700 kabla ya kuanguka katika bahari Magharibi mwa Japan.

Majaribio ya mara kwa mara ya makombora ya masafa marefu yanayofanywa na taifa hilo yanakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa na yamesababisha wasiwasi miongoni mwa jamii ya kimataifa pamoja na Marekani.

Marekani na Japan zimetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne.

Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA, limesema kwamba jaribio la kombora jipya la masafa marefu la Hwasong 12, lililenga kuonyesha kwamba kombora hilo jipya lina uwezo wa kubeba kichwa cha Nyuklia.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )