Saturday, May 6, 2017

Lowassa awalilia wanafunzi Waliofariki katika Ajali........Maiti 32 zapelekwa mochwari katika Hospitali ya Lutheran Karatu.

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ametuma salamu za rambi rambi kutokana na tukio la watu 32 kufariki dunia katika ajali ya basi.

Waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi Karatu, ni wanafunzi 29, walimu wawili, pamoja na dereva wa gari hilo.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo, ni ajali mbaya ambayo inaifanya siku hii kuwa mbaya katika historia ya nchi yetu,”alisema

Miongoni mwa wanafunzi waliofariki ni pamoja na wanaume 11 na wasichana 18.

Kadhalika maiti 32 zikiwamo za walimu wawili, dereva mmoja na wanafunzi 29 zimepokelewa sasa hivi katika Hospitali ya Lutheran Karatu.


==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )